MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, September 5, 2014

TUME YA UCHUNGUZI WA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI YAANZA RASMI KUPOKEA TAARIFA NA MALALAMIKO KUHUSU UTEKELEZAJI WA OPERESHENI TOKOMEZA NCHINI

Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza ujangili inatoa taarifa kwa umma kuwa imeanza rasmi kupokea taarifa na malalamiko mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili nchini.

Katika kufanikisha majukumu yake, Tume itatembelea maeneo mbalimbali nchini ili kukutana na wananchi wenye tarifa au malalamiko kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.

Aidha, Tume inawaarifu wananchi kuwa taarifa au malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni hiyo yatapokelewa kwa njia ya posta, barua pepe na simu za mkononi kama ifuatavyo;
i.                    Katibu wa Tume,
Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili,
SLP 9050,
Kivukoni Front,
Dar es Salaam

ii.                  Barua pepe: opereshenitokomeza@agctz.go.tz
iii.                Namba za simu
Tigo:                0714 826826
Vodacom:       0767 826826
Airtel:              0787 826826
Zantel:             0773 826826

Imetolewa na:
(signed)
Fredrick K. Manyanda
KATIBU WA TUME

No comments:

Post a Comment