MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, August 29, 2014

MAKALLA AWAPA UHAKIKA WA KUPATA MAJI WANAKIJI WA KIJIJI CHA CHAKWALE GAIRO MKOANI MOROGORO

Wananchi wa kijiji cha Chakwale watapata huduma ya maji ikiwa ni agizo la Rais jakaya kikwete alilolitoa juzi tarehe 26 akitokea kilindi kuelekea Gairo ambapo wananchi wa kijiji hicho walimsimamisha na kumuomba awapatie maji na katika kujibu alimuagiza Naibu waziri maji Amos makalla kufika kijijini hapo jumamosi tarehe 30 bila kukosa
Katika kutekeleza agizo hilo
Jana Naibu waziri wa maji Amos makalla alifika na kufanya mkutano wa hadhara na kuwakemea viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Killosa kwa kukaana hela za mradi wa maji wa kijiji cha Chakwale na kusababisha kero ya maji kijijini hapo alisema"
Makalla alisema Nimesikitishwa na hii tabia ya ukiritimba,mmekalia fedha na urasimu maofisini na kuwasababishia matatizo wananchi nasema tabia hii ikome kwenu na watendaji wengine kote nchini"
Naibu waziri wa maji amewagiza viongozi wa wilaya ya Gairo kutoa fedha hizo na ndani ya wiki mbili wampate mkandarasi wa kutafiti na kuchimba kisima awe amepatikana.

Aidha wizara ya maji itapeleka fedha sh 300milioni kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji na mradi ukamilike mwezi Novemba na si vinginevyo

No comments:

Post a Comment