Kamati ya Nidhamu
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Oktoba 11 mwaka huu)
imesikiliza malalamiko yaliyowasilishwa mbele yake dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro.
Shauri hilo
limesikilizwa na wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti wake Wakili
Jerome Msemwa. Wajumbe wengine wa kamati hiyo waliosikiliza shauri hilo
lililowasilishwa na TFF ni Kitwana Manara, Kassim Dau na Nassoro Duduma.
Hivyo, Kamati hiyo
itakuwa na mkutano na waandishi wa habari kutangaza uamuzi wake juu ya shauri
hilo. Mkutano huo utafanyika Jumatatu ijayo mchana katika Ofisi za Shirikisho
lililopo katika jingo la PPF
1.
Kamati ya
Utendaaji imesikitishwa na taarifa za upotoshaji kuhusu kanuni mpya za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL), hivyo inaomba radhi kwa wadau ambao wameguswa na kusumbuliwa
na matukio hayo.
2
.Kufuatia matukio
hayo, Sekretarieti ya TFF kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, imefungua mashtaka
kwenye Kamati ya Nidhamu dhidi ya Dk. Damas Ndumbaro ambaye ni mjumbe wa Bodi
ya Ligi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba. Pia wadau wote
waliohusika na upotoshaji huo wakiwemo wafanyakazi wa TFF na Bodi ya Ligi
watashughulikiwa kulingana na nafasi zao.
3.
Kutokana na madai
ya klabu kuhusu vipengele kadhaa vya Kanuni za Ligi Kuu 2014/15, Kamati ya
Utendaji imepanga kukutana na viongozi wa klabu za Ligi Kuu siku ya Jumamosi,
Oktoba 18 mwaka huu ili kuwasikiliza na kushauriana kuhusu changamoto za
kikanuni na uendeshaji wa mashindano kwa ujumla.
4.
Kamati ya
Utendaji itaendelea kuboresha Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi (Governing
Regulations) ili kuweka uwiano wa utendaji na kuepusha tofauti kati ya Bodi ya
Ligi, vilabu na TFF. Aidha Kamati ya Utendaji itafanya kila linalowezekana
kuboresha ligi kwa kuijengea uwezo Bodi ya Ligi kwa lengo la kuwa na ligi
zinazoendeshwa kisasa (Professional Leagues).
No comments:
Post a Comment