Katika mkutano muhimu uliofanyika jioni
hii hapa mjini Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika pamoja na
Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo
ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo
Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu.
Katika mawasilisho yake katibu Mkuu
huyo aliwaeleza viongozi wa Benki ya Dunia kuwa ,anashukuru kwa ushirikiano
mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana
Tanzania katika kupiga hatua kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile
alisema kuwa pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo
ambalo lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti.
Hili amelieleza kuwa
linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo yanayohusu IPTL
kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano. “ IPTL haina
uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii inaathiri
utekelezaji wa kibajeti.”alisema. Aidha aliendela kueleza kuwa sera ya Benki ya
Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na hivyo kutaka baadhi ya miradi
isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni changamoto nyingine”.
Katika mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa
ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo.
Kwa mapendekezo haya mawili makubwa
kama yatafikishwa kwenye ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu
itapiga hatua kama ilivyojipangia. Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo
kwa mikono miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi
Ujumbe kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha
mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji
anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose Mkurugenzi
Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.
No comments:
Post a Comment