Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa
kushirikiana na Makumbusho ya Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) wameandaa maonyesho na mdahalo wa kukumbuka na kuenzi mchango wa Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kujenga, kutetea, kulinda na
kudumisha amani Duniani.
Maonyesho hayo ya
siku tano ambayo yatafunguliwa tarehe 13 na kumalizika terehe 17 mwezi huu
yatafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa
na Gallus Abedi ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere ilisema maonyesho hayo yatajikita zaidi kuonyesha picha,
nyaraka, vitabu, matukio na kazi mbalimbali zinazohusiana na Baba wa Taifa ambaye ni Rais wa Kwanza na
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania.
Mada zitakazotolewa
katika mdahalo utakaofanyika tarehe 17 ambayo ndiyo siku ya kilele
cha makumbusho hayo ni
misingi, utekelezaji na usimamizi wa kujenga, kulinda na kudumisha amani na
uchambuzi na mifano halisi ya Sera za utekelezaji wa misingi ya kujenga amani
kwenye Sekta mbalimbali za maendeleo.
No comments:
Post a Comment