Taasisi
ya Mwalimu Nyerere inapenda kutoa taarifa kwamba imeandaa mdahalo wa Pili wenye
lengo la kujadili umuhimu wa kuielewa
kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Mambo ya msingi yaliyomo katika Katiba
hiyo yataainishwa na kujadiliwa na
washiriki wa Mdahalo. Taasisi ya Mwalimu
Nyerere inapenda kusisitiza kuwa lengo la mdahalo si malumbano au makatazo:
Lengo ni kutoa fursa kwa washiriki wa mdahalo na wananchi kwa ujumla
kujielimisha kuhusu Katiba inayopendekezwa ili waweze kuielewa vizuri, na hivyo
kujiandaa kuipigia kura katika mazingira ya uelewa kwa kuzingatia dhamira yao,
bila kulazimishwa, kutishiwa au hata kulipwa fedha na mtu au kundi lolote. Hakuna kiingilio katika mdahalo huo, na watu
wote wanakaribishwa.
Mdahalo
utafanyika kati ya saa 9.00 mchana na saa 12.00 jioni kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza,
Dar es Salaam. Washiriki wote wawe
wamefika Blue Pearl Hoteli saa 8 mchana.
2. Washiriki katika mdahalo
huo ni baadhi ya waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
wakiwamo Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph
S. Warioba, Mzee Joseph W. Butiku, Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bibi Mwantumu Malale, Mtumishi wa Umma
Mwandamizi Mstaafu, , Ndugu Awadh
Ali Saidi, Rais wa Chama cha Wanasheria
Zanzibar na Ndugu Humphrey Polepole, Mdau wa Maendeleo), Profesa Baregu, Jaji Mstaafu Mzee Ussi
(Zanzibar) na Ndugu Muhammad Mshamba (Zanzibar).wananchi na viongozi kutoka taasisi na asasi
mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za
kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari,
taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya
wafanyakazi, n.k. wanakaribishwa
kushiriki.
Imetolewa na:
Mkurugezi Mtendaji,
Taasisi ya Mwalimu
Nyerere,
S.L.P. 71000,
Fax No. : 255 22
2119216/2118354
India/Makunganya/Bridge
Street
1 Novemba, 2014
No comments:
Post a Comment