Mwakilishi Mkazi wa Benki
ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Philippe Dongier,
akipata maelezo kutoka kwa Said Ngosha Magonya, ambaye ni Kamishina
wa Fedha za Nje kuhusu utaratibu uliopangwa na Tanzania katika Mikutano hii ya
majira ya kipupwe.
Mikutano ya majira ya Kipupwe imeanza rasmi tarehe 14/4/2015 na
kuhudhuriwa na nchi mbalimbali wanachama zaidi ya 188. Mikutano hii huudhuriwa
na maelfu ya wafanyakazi kutoka serikalini, waandishi wa habari, Mashirika na
Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na kamati za kifedha.Taasisi
hizo kwa pamoja zitajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la
Fedha la Kimataifa.
Tanzania ni nchi wanachama katika
Mikutano hiyo.Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na
ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia
(WB), aidha Gavana wa Benki kuu Prof.
Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Hali ya
hewa mjini hapa ni baridi na manyunyu ya hapa na pale.
No comments:
Post a Comment