NA ingiaed Mduma washington DC
“Shirika
la fedha la kimataifa (IMF) hujishughulisha na kutoa ushauri wa kisera kwa nchi
wanachama na kutoa mikopo na misaada ya kifedha. Waziri wa Fedha Mhe. Saada
Mkuya Salum aliyaeleza hayo mjini hapa. Akishiriki kikao cha kundi la
Africa(African Group one Constituency). Kundi hili hukutana kila kunapokuwa na
mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia kwa lengo la
kuwezesha nchi za Afrika kuwa na sauti moja na kujua hatua ambazo Nchi za
Afrika zimefikia kuhusiana na Taasisi zake za kifedha.
Waziri wa Fedha wa
Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya ni Gavana katika mkutano huu akifuatiwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa
upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha
Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa
Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Katika Mkutano huu Magavana hawa ndio wenye maamuzi ya
juu na nguvu kubwa ya kuweza kuyashawishi mashirika ya kifedha kuhusu nini kifanyike.
Mkutano huu uliofanyika
leo, umeangalia uhalisia na vigezo vinavyotolewa na Shirika la Fedha la
kimataifa katika kuimarisha taasisi za kifedha katika nchi wanachama Afrika.
Katika
mkutano huu, mambo muhimu yaliyojadiliwani pamoja na maendeleo katika kundi
hilo na mabadiliko ya maboresho katika Benki ya Dunia. Wakijadiliana katika
mkutano huo wajumbe hao wameshauri Shirika la fedha la kimataifa pamoja na
taratibu zake, liangalie namna ya kulegeza masharti ya mikopo ili nchi
wanachama ziweze kufanya mabadiliko ya kifedha kwa urahisi.
Mikutano
hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. na nchi wanachama wanaendelea
kufika kwa wingi.
Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu
akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi la Afrika unavyoendelea. (African Group one Constituency)
No comments:
Post a Comment