Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa
wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa
masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.
Kwa mujibu wa
mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote
wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4,
2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.
Aidha, wanafunzi
wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao
kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and
Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo.
Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake
(http://olas.heslb.go.tz).
Pamoja na mambo
mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time
Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha
kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza
kujaza fomu za maombi.
“Waombaji wa mara ya
kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja
tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo
uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.
Aidha, mwongozo huo
umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika
taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.
Bodi imewasihi
waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote
wanapofanya na kuwasilisha maombi.
HESLB ilianzishwa
kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005
ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji
waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni
kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya
juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.
KILA
LA KHERI YANGA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini - TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la
kheri Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika
(CC) timuYoung Africans katika mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya Etoile
du Sahel utakaochezwa kesho nchini Tunisia.
Katika
salamu zake Malinzi amesema ,Young Africans wakiwa ndio timu wawakilishi pekee
wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa barani Afrika
wanapaswa kupambana kuhakikisha wanasonga mbele katia hatua inayofuata.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young
Africans ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile du Sahel, na mshindi wa jumla kwa
mchezo wa huo, atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa
zimetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.
Mchezo
huo wa marudiano utapigwa kesho jumamosi katika dimba la Olympique de Sousse
katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3 kamili usiku kwa saa za Afrika
Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment