katika
kutoa mafunzo ya usimamizi wa mambo ya uchumi kwa watendaji wa nchi wanachama.”
Aliendelea kusema kuwa katika siku hizi mbili wamekutana na chombo hicho kwa madhumuni
ya kuzungumzia maendeleo ambayo yanatokana na rasilimali kama vile gesi na
madinii na kutoa mapendekezo ya namna gani Afrika inaweza
kusimamia rasilimali hizo.
Akitoa
ufafanuzi katika majadiliano hayo Dr. Likwelile alisema”Tanzania kuna
rasilimali nyingi kama vile gesi ambayo imegunduliwa Mtwara na kusisitiza kuwa
kuna nchi Katika kipindi hiki cha mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha la Kimataifa, kumekuwa na mikutano mbalimbali inaendelea hapa
nchini Peru. Mikutano hiyo inaendeshwa na Taasisi mbalimbali zenye utaalamu wa
kiuchumi na kifedha. Akizungumza na waandishi wa habari, katibu Mkuu Wizara ya
fedha Dr. Servacius Likwelile alisema “MEFMI ni chombo kikubwa kwa Afrika
Mashariki na Kusini mbalimbali barani
Afrika ambazo zina dhahabu ya kutosha ambayo inaweza kuinua uchumi wa Afrika
kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuzitumia.
“Lengo
kuu la mkutano wa MEMFI ni kuzungumzia shughuli zinazofanywa na MEMFI ili
kuwezesha kupanga namna ya kuboresha uwezo na kuendesha shughuli zetu katika
kuinua uchumi wa Afrika kwani tutahitaji fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza
kwenye miundombinu lakini lazima tuhakikishe kwamba tunafanya hivyo ili
kuhakikisha uchumi wetu unakuwa imara na kunakuwa na utaratibu wa kuweka akiba kwa
ajili ya vizazi vijavyo, hili ni suala la msingi sana” alisistiza Likwelile.
Likwelile
aliongeza kuwa “Vizazi vingi vinatumia rasilimali zote bila kuangalia utaratibu
wawakati ujao kuwa utakuwaje, hivyo katika kikao hiki tumekubaliana kuanzisha
mfuko ambo ni kwa ajili ya kuwekeza kwa ajili ya matumizi ya baadae (Sovereign
Wealth Fund). Masharti ya mfuko huoyatakuwa ni kama ifuatavyo: (i) Mfuko huo
lazima uweze kuzalisha ajira, (ii)Mfuko huo lazima uwe na misingi imara ya
kusimamia uendeshaji wa shughuli zake,(iii) Mfuko lazima uwe na chombo imara
kinacho kisimamia mfuko huo. (iv) Lazima kuwe na utaratibu ambao unasema mfuko
huu utafanya nini na hautafanya nini.
La msingi
kuwe na mfumo wa kisheria lakini tuangalie rasilimali watu ili kuweza kuhifadhi
mfuko huo. Na namna gani miundombinu itawezakusaidia kuimarisha uchumi ili
uweze kutambuliwa.”
Naye
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu alisema kuwa,ni muhimu kujua
mapato yetu yatokanayo na upatikanaji wa madini kwani tunaweza kuyatumia vizuri
katika kuhakikisha tunatengeneza miundombinu, kuongeza uwezo wa kuzalisha na
baada ya hapo nchi iweze kuendelea kupiga hatua hata kama madini yatakuwa
yamekwisha.
Waziri wa
Fedha ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana
msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu
Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la
Kimataifa(IMF).
No comments:
Post a Comment