Agizo la Rais John Magufuli alilolitoa la kufanya usafi siku ya Uhuru Desemba mwaka jana limeitikiwa na wananchi wengi kote nchini
Sote ni mashahidi Rais kwa
mamlaka aliyonayo aliamua kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru na yeye
mwenyewe kuamua siku hiyo hiyo iwe ni siku ya kufanya usafi nchini kote nay eye
mwenyewe kushiriki katika eneo la Feri lililopo karibu na Ikulu ya Dar es
Salaam
Tulishuhudia siku hiyo viongozi mbalimbali akiwemo, Rais
mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete naye aliungana na watanzania kufanya
usafi eneo la Msoga Chalinze mkoani Pwani.
Mpaka sasa swala la kufanya usafi linaendelea kama
tulivyoambia na Wizara husika inayoshulikia mazingira kwamba kila jumamosi ya
mwisho wa mwezi itakuwa rasmi siku ya kufanya usafi
Maana yake ni kwamba
kila mtaa, kata, tarafa watakuwa wamejipanga ni kwa namna gani
wanavyolishughulikia swala la usafi ili kuona mazingira yanakuwa safi
Sasa tatizo lililopo
ni kwamba kweli watu wanashiriki katika swala la usafi kwa kuzikusanya taka
ambazo baadaye huwa zinatakiwa kubebwa kupelekwa dampo, lakini mara nyingi
utembeapo katika barabara zetu unakuta taka zimerundikwa unaweza ukaambiwa hizi
taka sasa ni wiki kutoka zilundikwe hapa, kazi iliyobaki ni kwa viongozi wa
mitaa kuweka utaratibu wa kuzibeba na kuzipeleka kunakohusika lakini bila kufanya
hivyo tatizo la uchafu litarudi palepale
No comments:
Post a Comment