Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Elijah Mwandumbya akizungumza na waandishi wa habari
alipotembelea kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya
usajili wa walipakodi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu kampeni ya usajili wa
walipakodi inayofanyika nchi nzima kwa lengo la kuongeza idadi ya walipakodi,
kupanua wigo wa ulipaji kodi na kuongeza mapato ya Serikali.
Mfanyakazi
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (kulia) Regina Urio akimhudumia mfanyabiashara
aliyefika katika kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho wa
Mlipakodi (TIN).
TRA YARAHISISHA USAJILI WA WALIPAKODI.
Na: Veronica Kazimoto,
Dar es Salaam.
Wafanyabiashara
wanaostahili kulipa kodi kwa njia ya makadirio, watalipa robo ya kwanza ndani
ya siku tisini (90) kuanzia siku waliyosajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo
wa kulipa kodi hiyo kabla mfanyabishara hajaanza kufanya biashara husika.
Hayo yamesema leo na
Kamishna wa Kodi za Ndani Elijah Mwandumbya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
alipotembelea kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni ya
usajili wa walipakodi.
Kamishna Mwandumbya
amesema kuwa, hapo awali wafanyabiashara walitakiwa kulipa robo mwaka ya kwanza
mara baada ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) suala
lililosababisha baadhi ya watu kushindwa kulipa kutokana na msingi mdogo wa
biashara zao.
"Niseme tu kwamba,
TRA tumeamua kuboresha huduma zetu kwa kuhakikisha kuwa, walipakodi wapya wanalipa
makadirio yao ndani ya miezi mitatu tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo
mfanyabiashara alitakiwa kulipa kabla ya kuanza biashara yake", alisema
Mwandumbya.
No comments:
Post a Comment