Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NIC, Mick Karima akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja
Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NIC (kushoto) akiwaongoza wateja wa benki hiyo kuchukua futari
Wafanyakazi na wateja wa benki ya NIC wakichukua futari
Wafanyakazi wa benki ya NIC na wateja wa benki hiyo wakipata futari
Wateja na wafanyakazi wa benki ya NIC wakifuru futari iliyoandaliwa na benki ya NIC
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NIC
Natasha akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NIC, Mikc Karima
Sunday, June 10, 2018
Sunday, April 15, 2018
TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA
Ofisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Lameck Ndida akitoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kwa wafanyabiashara
wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika
mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya
kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko,
changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa
wa Geita James Jilala (kulia) akijadiliana jambo na Meneja wa Huduma na
Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu, Gabriel Mwangosi wakati wa kampeni
maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa
wiki mkoani Geita. Katikati ni Afisa wa Kodi Mwandamizi wa TRA Makao Makuu
Maternus Mallya
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
wakiwasajili wafanyabiashara wapya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa
kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni
mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi,
kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na
maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao. Picha zote na Veronica Kazimoto
Na
Veronica Kazimoto,
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) imesajili jumla ya wafanyabiashara wapya 600 katika kampeni
maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyofanyika mkoani Geita ikiwa
na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza
malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Akizungumza mara baada
ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Menenja wa TRA mkoani hapa
James Jilala ameishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa kufika
mkoani Geita hususani katika maeneo ambayo hakuna ofisi ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi ndani ya wiki moja.
"Nianze kwa
kuishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa hatua ambayo mmeifanya ya
kufika katika Mkoa wetu wa Geita hasa maeneo ambayo hatuna ofisi ya TRA na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi kwa
muda mfupi kitu ambacho kimekuwa historia kwetu," alisema Jilala.
Jilala alisema kuwa,
baadhi ya wafanyabiashara walishindwa kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa
wakati, kwasababu walitakiwa kusafiri zaidi ya kilomita 100 kwenda Geita mjini
kwa ajili ya kupata huduma hiyo. Hivyo, zoezi hili limewarahisishia
wafayabiashara kusajiliwa na kupatiwa TIN.
Naye Meneja wa Huduma
na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu
Gabriel Mwangosi alisema kuwa , pamoja na usajili wa wafanyabiashara
hao, shughuli mbalimbali zimefanyika katika kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na
utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kupitia
semina na kuwatembelea katika sehemu zao za biashara.
"Katika zoezi hili
tumefanya shughuli nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wafanyabiashara
mahali wanapofanyia biashara zao, tumesajili wafanyabiashara wapya na tumetoa
semina mbalimbali ambazo tunaamini
kabisa zitakuwa zimebadilisha mtizamo,
utendaji na mwenendo mzima wa ulipaji kodi katika Mkoa huu wa Geita,"
alieleza Mwangosi.
Kampeni ya huduma na
elimu kwa mlipakodi ni moja ya mikakati ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania
imejiwekea katika kuhakikisha kuwa inasajili wafanyabiashara 1,000,000 katika
mwaka huu wa Fedha wa 2017/18.
Subscribe to:
Posts (Atom)