MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Tuesday, September 12, 2017

TUME YA HAKI ZA BINADAMU YAMPONGEZA JPM
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu,  Bahame Tom Nyanduga,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea tamko la  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Septemba 11, 2017 kuhusu kutotekeleza adhabu ya kifo wakati wa uongozi wake, kuwa ni tamko lenye kuzingatia haki ya msingi ya kuishi.
 Tume inapenda kuungana na wadau wengine kumpongeza  Rais kwa tamko hilo ambalo limekuja muda mfupi kabla ya Siku ya Kimataifa ya kuhamasisha nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuta adhabu ya kifo, ambayo huadhimishwa Oktoba 3 ya kila mwaka. 
 Uamuzi wa  Rais unaendana na Mkataba wa Kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa yanayozitaka nchi wanachama kufuta au kusimamisha utekelezaji wa adhabu ya kifo (abolition/moratorium on the death penalty).
 Tume inatambua kwamba adhabu ya kifo haijatekelezwa hapa nchini katika kipindi cha takriban miaka 20 iliyopita na hivyo kudhihirisha kwamba Tanzania ni nchi isiyotekeleza adhabu ya kifo kwa hiari yake yenyewe pamoja na uwepo wa adhabu hiyo katika sheria za nchi.


Kwa kuzingatia kauli ya Rais pamoja na mahitaji ya sheria za kimataifa za haki za binadamu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inapenda kuchukua nafasi hii, kuishauri Serikali iridhie Itifaki ya pili ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa; Itifaki ambayo inazitaka nchi wanachama kufuta adhabu ya kifo.


Wednesday, September 6, 2017

Wanamchi wajitokeza kupima afya bure jijini Dar es Salaam

 Wamamchi wakiingia kwenye viwanja ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kupima afya bure leo

Wanakishubiri huduma ya kupima afya bure katik viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo

Monday, August 7, 2017

Ziara ya Rais Dk John Magufuli, Korogwe mkoani Tanga

Muonekano wa Kituo kipya na cha kisasa cha mabasi alichokizundua Rais Dk John Magufuli akiwa katika mwendelezo wa ziara mkoani Tanga


Rais  Dk John Magufuli leo amezindua Kituo kipya na cha  kisasa ya mabasi mjini Korogowe mkoani Tanga

Maonyesho ya Nanenane kanda ya kati mkoani Dodoma


Ofisa Habari wa Bunge, Patson Sobha akizungumza na wanafunzi wa  Shule ya Msingi ya Maria de Mattias iliyopo kisasa Mjini Dodoma walipotembelea Banda la Bunge wakati wa Maonyesho ya Nane nane yanayoendelea   kwenye Viwanja vya Nzunguni, Mjini Dodoma