Chama cha waandishi wa habari za Mazingiara (Jet) kitafanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho jijini Dar es Salaam saa tatu kamili asubuhi juu ya alama. Usajili wa wajumbe wa mkutano utaanza saa mbili kamili asubuhi. Tafadhali tuwahi ili shughuli ianze mapema na tumalize mapema.
Mtakumbuka kuwa nimewasiliana nanyi mara tatu nikiwakumbusha wote kuthibitisha kuhudhuria mkutano ili sekretariati ya JET iweze kuandaa yale ambayo wajumbe wanapaswa kupata. Idadi ya waliothibisha ni 44, hivyo sekretariati imejiandaa kwa ajili ya kuhudumia idadi hiyo.
Wale wanachama hai ambao hawakuthibitisha kuhudhuria mkutano
wanakaribishwa, lakini stahili nyingine hazitawahusu, kwa maana ya kulipwa nauli posho na kadhalika.
Naomba kuwasilisha.
MKUTANO MKUU WA MWAKA
2013
WALIOTHIBITISHA KUUHUDHURIA
NO.
|
JINA
|
MKOA
|
NAMBA YA SIMU
|
1.
|
Felix Endrew
|
D’Salaam
|
|
2.
|
Dr. Ellen Ockedion
|
D’Salaam
|
0784 401884
|
3.
|
Chrysostom Rweyemamu
|
“
|
0713 329005
|
4.
|
Gerald Kitabu
|
“
|
0713 612698
|
5.
|
Johnson Mbwambo
|
“
|
0754 564916
|
6.
|
Harieth Kiwale
|
D’Salaam
|
|
7.
|
Ludger Kasumuni
|
D’Salaam
|
0754 458911
|
8.
|
Travena Maimu
|
D’Salaam
|
|
9.
|
Upendo Mwinchande
|
D’Salaam
|
0652 487457
|
10
|
Janet Shekunde
|
D’salaam
|
|
11
|
Sekela Mwambuli
|
D’Salaam
|
0758 405474
|
12
|
Aisha Dachi
|
D’Salaam
|
0754 467133
|
13
|
Judica Losai
|
“
|
0713357713
|
14
|
Deodatus Mfugale
|
“
|
0754 275170
|
15
|
Sidi Mgumia
|
“
|
0714 327572
|
16
|
Endrew Chale
|
“
|
0719 076379
|
17.
|
Josefu Lino
|
“
|
0712 431537
|
18.
|
Antony Siame
|
“
|
0713 403248
|
19.
|
Stella Barozi
|
“
|
0718 194414
|
20.
|
Christina Mokimilya
|
“
|
0715 686705
|
21.
|
Simon Nyalobi
|
“
|
0785 345489
|
22.
|
Lucy Ogutu
|
D’Salaam
|
0713 540994
|
23.
|
John Chikomo
|
D’Salaam
|
0754 263965
|
24.
|
Mwanaharusi Pongwa
|
D’Salaam
|
0715 444792
|
25.
|
Felix Mwakyembe
|
Mbeya
|
0713 290487
|
26.
|
Brandy Nelson
|
Mbeya
|
0754 011770
|
27.
|
Jumbe Ismail
|
Singida
|
0754 080740
|
28.
|
Ali Hamad
|
Pemba
|
0777 458523
|
29.
|
Zainab Mwatawala
|
Morogoro
|
0655 423456
|
30.
|
Salome Kitomari
|
Moshi
|
0754 080740
|
31.
|
Ileje Env Conservation group
|
Mbeya
|
|
32.
|
Albano Midelo
|
Songea
|
0784 765917
|
33.
|
Ashton Balaigwa
|
Morogoro
|
0713 811110
|
34.
|
Haji Mohamed
|
Pemba
|
0777 870191
|
35.
|
Joseph Malembeka
|
Morogoro
|
0655 824151
|
36.
|
Fitina Haule
|
Morogoro
|
0754 654678
|
37.
|
Henry Mwakifuna
|
Ifakara, Morogoro
|
0764 516666
|
38.
|
Vedasto Msungu
|
Morogoro
|
0713 640700
|
39.
|
Nathaniel Limu
|
Singida
|
0755 417789
|
40.
|
Editha Karlo
|
Kigoma
|
0752 202783
|
41.
|
Anthony Kayanda
|
Kigoma
|
|
42.
|
Alisante John
|
Singida
|
|
43.
|
Esther Macha
|
Mbeya
|
0753 804343
|
44.
|
Jane Sume
|
Arusha
|
CHAMA CHA WAANDISHI WA
HABARI ZA MAZINGIRA TANZANIA
(JET)
(RIPOTI YA UTENDAJI FEBRUARI 25, 20012 – MACHI 2, 2013)
(RIPOTI YA UTENDAJI FEBRUARI 25, 20012 – MACHI 2, 2013)
1.0
Muhtasari
Kwa
kipindi cha mwaka mzima tangu mkutano mkuu ufanyike mwaka jana Februari 25
(2013), JET imetekeleza mambo kadhaa yakihusisha uchapishaji wa gazeti la Kasuku, kuhamasisha waandishi
kujiunga na JET, kutathmini uharibifu wa mazingira katika sehemu mbalimbali
nchini zikihusisha Bonde la Mto Kilombero ambalo limeharibiwa sana na wafugaji,
Mlima Kilimanjaro ambao uasili wake sehemu zenye misitu umeharibiwa mno pia;
tumetembelea pia mikoa ya Lindi, Mtwara na Pwani ambako misitu imefyekwa sana
bila utaratibu, na uvuvi haramu kuendelea kwa kasi katika mikoa hii.
Aidha,
tumetembelewa na wageni mbalimbali kutoka
hapa nchini na nje ya nchi, washirika mbalimbali wamekuja kwenye ofisi
za JET kuona namna ambavyo tunaweza kufanya kazi pamoja wakiwamo Mama Misitu
Campaign (MMC) na Revenue Watch Insitute inayojihusisha na uandishi wa masuala
ya gesi, mafuta na madini yenye makao makuu jijini New York, Marekani na ofisi
zake za kanda zikiwa jijini Accra, Ghana; na hivi karibuni Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) limeomba JET ifanye kazi kwa karibu nalo, hasa katika sehemu
za vyanzo vya maji ambavyo hatimaye hupeleka maji katika mitambo ya kufua umeme
huko Kidatu (Morogoro) na Mtera
(Iringa).
Pia
katika kipindi hiki hiki, JET imeweza kutengeneza documentary mbalimbali za
mazingira, imeshiriki katika kutoa maoni kuhusu Katiba mpya na tumeweza kuhamia
katika ofisi mpya zilizo Tegeta, Dar es Salaam (off
Bagamoyo Road,
Barabara ya Chanika mara baada ya kupita Kibo Commercial Complex kama unaelekea Bagamoyo). Kuhama huku kulitokana na
mwenye jengo tulikokuwa katikati ya jiji, Mnazi Mmoja, kututaka tuondoke.
2.0
Kwa ufupi, katika kipindi cha Februari 25, 20012 hadi leo
Machi 2 mwaka huu (2013), JET imejitahidi kwa uwezo wake kutekeleza majukumu
yaliyotajwa hapa chini:
·
Kusimamia
utekelezaji wa miradi mipya na ya zamani.
·
Kuandaa
safari za kikazi mikoani (field trips)
kwa waandishi wa habari
·
Kuandika
miradi mipya na kuiwasilisha kwa wafadhili
·
Kuandaa
na kuchapisha gazeti la Kasuku/JET News
·
Kuandaa
rasimu ya katiba mpya ya JET
·
Kushirikiana
na vyama vingine vya mazingira ndani na nje ya nchi
·
Kuhamasisha
waandishi zaidi kujiunga na JET
3.0 Miradi
3.1 Mradi wa Fredskorpset
ambao ni wa kubadilishana vijana wasiozidi miaka 35 kwa nchi za Tanzania,
Uganda, Kenya na Ethiopia uliendelea vizuri mwaka jana kwa mwaka wa 10
mfululizo, na unaendelea tena kwa mara ya mwisho mwaka huu.
Vijana
wetu, Jamilah Khaji na Sidi Mgumia walifanya vizuri huko Kenya na Uganda; na vijana waliopokewa nasi
pia walifanya vizuri. Adamu Mussa kutoka Uganda alifanya kazi kwenye gazeti la The Citizen na Nicholas Begisen kutoka
Kenya, ambaye alianzia kwenye gazeti la The African, alimalizia shughuli zake
kwenye gazeti la The Guardian.
Kama ilivyo
taratibu za mradi huu, kuanzia Julai 17 hadi 21 mwaka jana (2012) kulifanyika
mikutano ya Review na Planning kwa ajili ya maandalizi ya
mradi wa mwaka 2012/2013. Mkutano huo ulifanyika Kampala, Uganda.
Kwenye
mkutano huo, Mkurugenzi wa FK Africa Regional Office, Fikre Haile Meskel,
alitoa maelezo ya mabadiliko ndani ya FK Oslo. Mabadiliko hayo ni pamoja na
kubadilika kwa sera, mwonekano, bajeti, na ukomo wa ubadilishanaji wa
wafanyakazi.
Alieleza kuwa mabadiliko hayo ya kiutendaji na
kimfumo si tu yamebadilika huko Norway,
bali pia ni kwa wote wanaohusika katika mradi huu wa kubadilishana washiriki
(partners).
Alisema
kwamba tayari mitandao (networks) miwili, yaani AMPCAN pamoja na MEDIA WOMEN
zimekwisha kufikia ukomo wa kushiriki, na mtandao (network) unaofuata kufikia ukomo ni ya Environmental Journalists ambao sisi JET ndio tunauongoza. Kwamba sasa tumepewa
mwaka wa mwisho wa kushiriki katika mradi huu.
Maandalizi
ya mradi huu kwa mwaka 2012/2013 yalienda vizuri na tunaendelea vizuri. Tayari
tumepokea vijana wawili, mmoja kutoka EEJA, Ethiopia
na mwingine kutoka VCDO, Kenya.
Nasi tumepeleka vijana wetu wawili, mmoja RUDMEC nchini Uganda na mwingine VCDO nchini Kenya.
Mafunzo
ya wiki mbili yajulikanayo kama FK PREPARATORY COURSE kwa vijana waliochaguliwa
kushiriki kwenye mradi huu yalifanyika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini katika wiki
ya kwanza ya Novemba mwaka jana (2012). Vijana waliokwenda kwenye mkutano huo
walitoka Tanzania, Kenya, Uganda
na Ethiopia.
Katika kikao cha Kamati ya
Utendaji ya JET iliyokaa hivi karibuni ilijadili na kubungua bongo (brainstorm)
kuhusu mradi huu wa Fredskorpset ambao unakaribia kufika ukingoni, yaani mwaka
huu.
Mradi huu kwa muda mrefu ndio
ulikuwa unabeba shughuli za JET kwa asilimia 80, hivyo kulikuwa na ulazima wa
kujadili na kubungua bongo kuhusu njia nyingine mbadala za kuhimili shughuli za
JET baada ya Fredskorpset kufikia mwisho.
Baadaye ilibainika kuwa JET
inahitaji miradi mikubwa minne ili kuziba pengo litakaloachwa na Fredskorpset.
Aidha, Kamati ya Utendaji ilikubaliana kufuatilia plan B ya Fredskorpset,
kwamba taasisi moja moja inaweza kuomba yenyewe ufadhili wa Fredskorpset kama inaona ina hoja, na ikizingatiwa kwamba JET inaweza
kufanya hivyo kwa sababu suala la mazingira, hasa mabadiliko ya tabianchi
(climate change), ni muhimu na nyeti kwa sasa duniani kote.
3.2
Mradi wa Mama Misitu (Mama Misitu Campaign – MMC): Mradi
wa Mama Misitu ni wa miaka mitano – na umeanza kutekelezwa hivi karibuni katika
wilaya za Kilwa, Kisarawe na Kibaha. JET
ni mmoja wa washiriki (partners) kadhaa
wanaotekeleza mradi huu, sisi JET tukitekeleza mradi huu katika eneo la makala,
redio/TV programu na uchapishaji wa gazeti la Kasuku. Kabla ya kupewa mradi huu, sharti la wafadhili lilikuwa
kuwa ni lazima mratibu wa mradi (project co-ordinator) na mhasibu wa mradi
waajiriwe.
Hilo
limefanyika, na MMC waliweza kufanya ziara mbili katika ofisi za JET, moja
ikiwa ni wao kujitambulisha kwetu sisi kama
moja ya asasi zitakazotekeleza mradi.
Ziara
yao ya pili
ilikuwa ni kuangalia uwezo wetu kiutendaji na kifedha (Organisation Capacity na Financial
Capacity). Uzinduzi wa mradi huu
ulifanyika Julai 31 mwaka jana (2012).
3.3 Mradi wa “Advocacy and Awareness
Raising Campaign to Policy and Decision makers on the Effects of Dynamite
Fishing”
Mradi
huu ambao umefadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS) ni mradi wa
miaka mitatu kuhusu eneo la utawala bora na uwajibikaji.
Katika
kipindi cha Aprili hadi Julai mwaka jana, JET iliweza kutembelea vijiji vya
mkoa wa Mtwara na kufanya tathmini, kuongea na wadau WWF-Mtwara, BMU Msanga
Mkuu, Mnazi Bay Marine Park, Polisi mkoa na Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya
Mtwara ili kutathmini mwenendo wa uvuvi na kuandaa vipindi vya redio na kuandika
makala.
Mbali na tathmini hiyo,
tumeendelea kutoa makala mbalimbali juu ya hali halisi ya uvuvi wa kutumia
baruti, kuperemba (monitor) jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali,
changamoto, mafanikio, sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 na mambo ya kufanya ili
kurekebisha hali iliyopo.
Utekelezaji wa mradi huu umekwisha
kufikia karibu miaka miwili, hivyo mradi husika umebakiza mwaka mmoja wa
utekelezaji.
3.4 Mradi wa Climate Change:
Mradi huu
tayari umekwisha kufungwa rasmi. Mradi huu ulifadhiliwa na Tanzania Media Fund
(TMF) kwa mwaka mmoja, na kwamba technical report na audited report zote mbili
za JET zimepongezwa na TMF, hasa jinsi zilivyoandaliwa vizuri.
3.5
Uwezekano
wa kupata watu nje ya JET kuandika miradi kwa malipo kidogo:
Katika
harakati za kuandika miradi ili kutafuta fedha za kuendesha shughuli za JET,
tumeangalia uwezekano wa kupata watu kutoka nje ya JET kuandika miradi kwa
malipo kidogo. Tumefanya hivyo, na kwa kuanzia, tumeanza na mradi mpya wa
kwenda TMF.
3.6
Kuwatembelea
wafadhili kutafuta miradi/ Kuandika miradi mipya:
Kuhusu
suala la kuwatembelea wafadhili, tumeweza kufanya mazungumzo na Ubalozi wa
Uingereza, na kufanya appointments na Ubalozi wa Finland na Norway. Tunasubiri majibu baada ya wahusika kumaliza likizo
za Noel na mwaka mpya wa 2013.
Kuhusiana
na kuandika miradi mipya na kuiwasilisha kwa wafadhili, kazi kubwa iliyofanyika
katika kipindi kinachohusu ripoti hii, pamoja na kutekeleza na kusimamia miradi
iliyopo, ilikuwa ni kuandika miradi mipya na kuiwasilisha kwa wafadhili.
Miradi
iliyoandikwa ni “Training workshop on Reporting Climate Change”, “Climate
Change and Media Project” ambayo imewasilishwa BHC- Ubalozi wa Uingereza; na Mradi wa “Improved Livelihood
through Sustainable Land Management and Adaptation to Climate Change Impacts in
Drylands of Tanzania” ambao umewasilishwa Global Mechanism; na wa advocacy wa Reduced
Emmessions from Deforestation and forest Degradation – REDD utakaowasilishwa
TMF. Tumeshauriwa na TMF kuwa tuwasilishe mradi huu Aprili mwaka huu.
4.0 Marekebisho ya Katiba: Wahesimiwa
wana-JET, mtakumbuka kuwa katika mkutano mkuu uliopita wa Februari 25 mwaka
jana, moja ya maazimio yaliyofikiwa ni kurekebisha katiba ya sasa ya JET ili
iendane na wakati.
Baada ya azimio hilo, Kamati ya
utendaji ya JET ilikaa na kuteua mjumbe
wa Kamati ya utendaji, Zainabu Mwatawala (ambaye pia ni mwanasheria), kuipitia
katiba ya zamani na kuleta mapendekezo, kazi ambayo aliifanya vizuri, na
mapendekezo hayo yalitumwa kwa wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji, wakiwamo
wanachama wote, ili kuiboresha zaidi.
Inasikitisha sana kuwa ni mwanachama
mmoja tu aliyeleta mapendekezo yake, ukiondoa wajumbe wa Kamati ya Utendaji!
Rasimu ya katiba mpya inayopendekezwa itawasilishwa kwenye kikao
hiki
kwani ni moja ya dondoo
za ajenda.
5.0
Kushirikiana na wadau
wengine wa mazingira (networking)
Katika
kipindi hiki ambacho ripoti hii inahusika nacho, JET iliendelea kujenga
uhusiano wa kikazi na wadau mbalimbali.
Mbali
na kujenga uhusiano mzuri na Serikali, JET pia iliimarisha uhusiano na wadau wapya,
ikiwamo GM-Global Mechanism yenye makao makuu yake Rome, Italia, katika kitengo
maalumu kinachoshughulikia masuala ya majangwa.
Mdau
huyu mpya yupo katika harakati za kusaidia Serikali za Afrika pamoja na
mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoshughulika na masuala ya majangwa pamoja
na matumizi endelevu ya rasilimali ya ardhi.
Kama nilivyoeleza kwenye
muhtasari hapo juu, Mama Misitu Campaign (MMC), TANESCO na Revenue Watch
Insitute inayojihusisha na uandishi wa masuala ya gesi, mafuta na madini ni wadau
wetu wapya pia.
6.0
Tuzo ya
Mazingira ya JET (JET Environmental Award)
Mara
mbili huko nyuma – kwa miaka miwili mfululizo - JET iliweza kuwatuza waandishi
bora wa mazingira, na kukwama baadaye baada ya kukosa fedha za kuendeleza zoezi
hili, hususan baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kukwamisha zoezi
hili baada ya kuahidi fedha na kushindwa kuzitoa.
Baadaye
MCT ililidaka wazo hilo,
na sisi JET tukawa watazamaji bila kuhusishwa kikamilifu katika uteuzi wa
mwisho wa mshindi wa mazingira.
Kamati ya
Utendaji tayari imependekeza kuwa JET irudishe Tuzo ya Mazingira ya JET kwa sababu JET ni taasisi ya mazingira, na
kwamba hiyo ni ajenda yake, lakini wakati huo huo tuendelee na ushirikiano (partnership)
na MCT.
Sasa
mikakati na mpango kazi vinafanywa na Kamati ya Utendaji ya JET kwa kuratibiwa
na wajumbe wawili wa Kamati hiyo, Dk. Ellen Otaru na Gerald Kitabu, ili
kufanikisha zoezi hili. Mikakati ni pamoja
na kutengeneza documentary fupi ya mafanikio ya JET tangu kuasisiwa kwake
(successs story) na kuwekwa kwenye mfumo bora ambako inaweza kuuzwa kirahisi
kwa wafadhili watakaochaguliwa/kuteuliwa kwa makini.
Orodha ya wafadhili hao
inaandaliwa na italetwa kwenye kikao kijacho cha Kamati ya Utendaji kwa ajili
ya kuhakikiwa na kuanza kufanyiwa kazi.
7.0 Kuhamasisha
waandishi zaidi kujiunga na JET
Tangu kufanyika kwa
mkutano mkuu mwaka jana Februari 25, wanachama wapya 37 wamejiunga na JET. JET
pia inaendelea kuhamasisha wanachama wengine wajiunge, na inaendelea kupokea
maombi mapya. Kamati ya Utendaji ya JET hukaa na kupitia maombi hayo na
kupitishwa kama yakikidhi vigezo. Wanachama
wapya 13 wamepitishwa na Kamati ya Utendaji kuwa wanachama mwezi uliopita
(Februari 9, 20013).
7.1
Hali ya michango (ada) ya wanachama ya JET
Mojawapo
ya jukumu la wanachama kwa JET ni kuhakikisha kuwa wanalipa michango yao kwa wakati ili kukipa
kani (nguvu) chama chao. Kama ambavyo tumekuwa
tukiwataarifu kwenye taarifa ambazo Katibu Mkuu amekuwa akiwaletea mara kwa
mara, baadhi yetu hatutimizi wajibu wetu ipasavyo kwa JET.
Waheshimiwa
wana-JET, kama mnavyojua, wafadhili wengi hutumia kigezo cha ulipaji ada kama mojawapo ya vigezo katika kufadhili miradi
inayowasilishwa kwao.
Kwa
kweli hali ya michango inasikitisha. Miongoni mwa wanachama wote wa JET wenye
ithibati, kwa maana ya kuwa wanachama wa zamani, ni wanachama 26 tu ambao
wametimiza majukumu yao kwa JET kwa kulipa michango yao kwa wakati. Wana-JET
waliobaki wanadaiwa michango yao,
na wana-JET 28 wamekwisha kufa kichama kwa kutimiza au kuzidi miaka miwili bila
kulipa ada zao.
Kwa
maana hiyo hawa si wanachama tena na wataondolewa kwenye orodha ya wana-JET! Katiba
ya JET iko wazi. Inasema kuwa mwanachama
anakufa kichama akilaza michango yake kwa muda wa miaka miwili mfululizo.
Wanachama ambao wamekufa kichama, wanaruhusiwa kuomba uanachama upya.
Katika
hali hii, sekretariati ya JET inawaomba wote mtoe michango yenu ili mkipe nguvu
chama chenu kipate urahisi wa kutekeleza majukumu yake, ukiwamo kuupa uanachama
wenu uhai kikatiba, hasa wale ambao wako pembezoni kufa kichama.
8.0 Kiwanja cha JET
Kiwanja
ambacho JET ilikuwa inafuatilia maeneo ya Mbweni JKT mwaka jana, mwenye kiwanja
hicho aliendelea kutaka bei kubwa. Hivyo JET iliamua kufuatilia kiwanja kingine
wilayani Kibaha ambako nako viwanja vingi tayari vilikuwa vimekwisha kuuzwa.
Eneo lililokuwa limebaki ni viwanja vilivyo eneo la Jisunala, Mlandizi ambako
maeneo yaliyotengwa ni kwa ajili ya shule na hospitali; na sehemu iliyokuwa
imebaki kwa ajili ya ofisi ni ndogo mno, yaani sq m 4,500, ambayo pia iko
umbali wa kilomita yapata 10 kutoka barabara ya Morogoro. JET haijakata tamaa,
inaendelea na juhudi za kutafuta kiwanja kitakachokidhi mahitaji ya JET ya
baadaye. Uharaka wa kukipata pia utategemea upatikanaji wa fedha kwa ajili ya
shughuli hiyo.
9.0
Changamoto
9.1 Katika kipindi cha mwaka mmoja, kama
ilivyokuwa miaka ya nyuma, mojawapo ya changamoto kubwa ilikuwa upatikanaji wa
wanachama wa kutekeleza kazi mbalimbali kukidhi matakwa na viwango mahususi vya
wafadhili. Hatutaki kutoa lawama kwa yeyote kwani wanachama wengi wameajiriwa
na vyombo mbalimbali vya habari, na hivyo kuwajibika kwanza kwa waajiri wao.
Hata
hivyo, baadhi ya wale waliopewa kazi, ama walichelewa kuzifanya, au wamezifanya
chini ya kiwango au wengine hawakufanya kabisa! Hali hii imetupa kazi kweli na
ugumu wa kuripoti kwa waliotoa fedha za kazi hizo, na mwisho wa siku kubomoa
sifa ya JET machoni mwa wafadhili hao!
Kwa
hali hiyo, tunawaomba sana wale ambao tutatakiwa kufanya kazi za chama, tuwe
tayari kuzifanya kwa ufanisi mkubwa.
9.2 Kuna baadhi ya wafadhili ambao huchelewa
kutoa fedha, hivyo kuathiri utekelezaji wa shughuli za miradi na kuifanya JET
kuwa na wakati mgumu kuandika ripoti za miradi hiyo katika muda uliobana.
9.3 Changamoto nyingine ni mawasiliano kati ya
wanachama na uongozi. Uongozi umekuwa ukiwasiliana na wanachama kwa kuwajuza
yanayojiri JET mara kwa mara. Lakini mrejesho kutoka kwa wanachama umeendelea
kuwa haba hasa!
Mfano
mzuri ni agizo lililotolewa na wanachama kwa uongozi wa JET katika mkutano mkuu
wa chama uliopita kuhusu mabadiliko ya katiba mpya. Mapendekezo ya mabadiliko
hayo yalifanywa na uongozi wa JET na kutumwa kwa wanachama wote kwa ajili ya
kuchangia. Ni mwanachama mmoja tu aliyeleta mrejesho, tena baada ya kutoa
kumbusho!
Katika
hali kama hiyo, wakati mwingine uongozi unashindwa kujua kama taarifa zilifika
kwa wanachama au vinginevyo! Waheshimiwa wana-JET, inatosha tu kutuambia “asante kwa taarifa”, angalau tukajua kuwa ujumbe
umefika kama wachache wenu, wachache kwa maana
ya kuwa wachache, wanavyofanya.
9.4 Uandikaji na ufadhili wa
miradi: Uandikaji na ufadhili wa miradi ni kazi ngumu kufanikisha, hususan
linapokuja kumpata mtu kufadhili miradi hiyo. Kuandika miradi kunahitaji
uweledi katika eneo hilo,
na pia kuuza miradi iliyotayarishwa kunahitaji mkakati yakinifu na diplomasia
isiyo haba.
10.0
Ofisi mpya za JET
Mtakumbuka
kuwa tuliwaletea taarifa ya ofisi za JET kuhamia Tegeta kutoka Mnazi Mmoja
katikati ya jiji. Hivi sasa ofisi hizo zipo Tegeta, Barabara ya Chanika yapata
mita takriban 200 kutoka Barabara iendayo Bagamoyo. Barabara hii ipo baada ya
kupita Kibo Commercial Complex upande wa kulia kama
unaelekea mjini Bagamoyo.
Ilikuwaje
tukahama? Mwenye nyumba ambako ofisi za JET zilipokuwa kwa zaidi ya miaka 20
alitaka kuhamia mwenyewe kwenye ofisi hizo baada ya yeye kuambiwa pia ahame kwenye ofisi alizokuwa anapanga.
JET
ilijaribu kutafuta ofisi nyingine katikati ya jiji haikufanikiwa. Ofisi
nyingine zilizopatikana maeneo ya Makumbusho na Sinza, ama zilikuwa ghali sana kiasi kwamba JET
tusingeweza kumudu gharama zake au zilikuwa chini ya kiwango. Ofisi za Tegeta
ni nafuu na zinaridhisha. Tayari Kamati ya Utendaji ya JET imekwisha kufanyia
mkutano wake mmoja kwenye ofisi hizo mpya.
11.0
Mwelekeo wa Chama kwa
mwaka 2013
Mbali na
kuendelea na kazi ya kuimarisha uwezo wa chama kiutendaji (capacity building),
pamoja na kufanya kazi kwa uwazi kama ambavyo JET imekuwa ikifanya, shughuli
kubwa zinazotarajiwa kufanywa mwaka huu ni:
·
Kusimamia
utekelezaji wa miradi mipya na ya zamani, ukiwamo wa Fredskorpset, MMC na ule
unaofadhiliwa na Foundation for Civil Society (FCS).
·
Kuandaa
na kuandika miradi mipya
·
Kuandaa
safari za kikazi (field trips) nne za mikoani na kuandika makala za viwango
·
Kusimamia
utoaji wa gazeti la Kasuku na JET News (baada ya kupata ufadhili)
·
Kuandaa
press conferences katika maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani, Siku ya Mazingira
Duniani na Siku ya Makazi Duniani
·
Kuhamasisha
wanachama kulipa michango yao
kwa wakati; na kuwahamasisha waandishi zaidi kujiunga na JET
12.0 Bajeti ya JET kwa mwaka 2013
12.1 JET
imekuwa ikiendesha shughuli zake kwa kutegemea vyanzo mbalimbali vya
mapato.
Mapato hayo
hutokana na michango ya wanachama wake, fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali;
na fedha zitokanazo na utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Mwanzoni mwa
mwaka 2012, Bajeti iliyopitishwa ilikuwa kama ifuatavyo:
·
Mapato Sh 257,107,960.00
·
Matumizi Sh 253,243,488.69
·
Baki Sh 3,864,471.31
Kwa sababu baki la mapato baada ya matumizi
ilikuwa ni Sh 3,864,471.31 tu, Kamati ya Utendaji iliagiza kwamba bajeti
iendane na makadirio ya mapato na kufuata matumizi kama kasma zinavyoonesha. Aidha,
Kamati hiyo ilipitisha mapendekezo ya Bajeti baada ya kuifanyia marekebisho.
12.2 Mwendo wa bajeti hadi Desemba 2012
Kwa
ujumla mwenendo wa bajeti katika kipindi chote cha mwaka (2012) ulikuwa ni wa
kuridhisha. Pamoja na kwamba matumizi hayakuzidi mapato, matumizi ya baadhi ya
miradi mbalimbali yaliweza kugharimiwa kutokana na mapato hayo hayo
yaliyotokana na miradi iliyofadhiliwa.
12.3 Bajeti ya 2013
a) Mapato
Fredskorpset:
Kufika
Desemba 31 mwaka huu (2013), tunatarajia kasma hii kuingiza kiasi cha Sh 165,387,200. Hili ni eneo ambalo linatuletea mapato ya
uhakika, na ni mradi ambao unachangia zaidi ya asilimia 80 ya pato la chama.
Foundation
for Civil Society:
Mapato katika kasma hii yanatarajiwa kuwa Sh 52,618,000.
Mama
Misitu Campaign:
Mapato katika kasma hii yanatarajiwa kuwa kiasi
cha Sh 65,998,000.
Michango kutoka
kwa wanachama:
Mapato
yatokanayo na kasma hii, wanachama wakitoa michango yao kwa wakati, yanaweza kufikia Sh. 6,000,000.
Hivyo kwa ujumla, mapato ambayo tunatarajia kukusanya mpaka mwisho wa
mwaka ujao wa fedha, ambao ni Desemba 31 mwaka huu (2013) ni jumla ya fedha za
Kitanzania Sh 290,003,200 kwa mchanganuo ufuatao:
-
Sh
284,003,200 kutokana na miradi; na
-
Sh
6,000,000 yakiwa makusanyo ya michango ya wanachama wetu.
-
Mradi wa Fredskorpset utaleta kiasi cha Sh 165,387,200
(USD 103,367). Tunatarajia kubana matumizi ya Sh 48,000,000 (USD 30,000) ambazo
zinaingizwa katika kasma za matumizi ya ofisi, hivyo kubakiwa na Sh 117,387,200
(USD 73,367) kwa ajili ya kuendesha shughuli za mradi mpaka mwisho wa mwaka huu
wa 2013.
-
Foundation for Civil Society: Katika mradi huu
tunatarajia kupata kiasi cha Sh 52,618,000 kwa kipindi cha mwaka mzima; lakini
tumetengewa fedha za kuendesha ofisi kiasi cha Sh 10,478,000; hivyo kubakiwa na
kiasi cha Sh 42,140,000 kwa ajili ya kuendesha shughuli nyingine za mradi kama
inavyoainishwa na mchanganuo wa mapato na matumizi.
- Mama Misitu Campaign: Katika mradi huu tunatarajia kupata kiasi cha Sh 65,998,000
kwa kipindi cha mwaka mmoja, lakini fedha kiasi cha Sh 19,678,400 zimetengwa
kuendesha gharama za ofisi, hivyo kubakiwa na Sh 46,319,600 kwa ajili ya
kuendesha shughuli nyingine za mradi kama inavyooneshwa katika mchanganuo wa
mapato na matumizi.
Kwa msingi huo, tunatarajia kupata jumla ya Sh 84,156,400 kama fedha za kuendesha
shughuli za ofisi kutoka katika kasma tofauti kama ifuatavyo:
·
Sh 48,000,000 kutoka
Fredskorpset
·
Sh 10,478,000 kutoka
Foundation for Civil Society
·
Sh 6,000,000 kutoka
kwa Michango ya ada ya wanachama
·
Sh
19,678,400 kutoka
Mama Misitu Campaign
Maelezo
ya kina kuhusu suala hili yatafafanuliwa na idara ya Uhasibu/Mkurugenzi.
13.0 Hitimisho
Waheshimiwa
wana-JET, naomba mniruhusu nichukue nafasi
hii, kwa niaba ya uongozi wa JET, niwashukuru sana wale wanachama wachache
walioitikia wito wetu wa kujenga tabia ya kupitapita JET kabla ofisi hazijahama
kutoka mjini ili kujionea jinsi chama chenu kilivyokuwa kinaendelea, matatizo
yaliyokuwa yanakisibu na kutoa ushauri, ukiwamo wa namna ya kutafuta fedha
(fund raising) kwa ajili ya kuendesha shughuli za JET.
Na
wale ambao hawakupita, nao si vibaya nikiwashukuru kwa kututakia mema katika
shughuli za chama chenu. Basi mwaka huu jenga tabia ya kupitapita mara kwa mara
JET ili muipe sekretariati nguvu ya kusukuma mbele chama kwa kasi zaidi.
Nawashukuru
sana tena, na naomba kuwasilisha.
Chrysostom Rweyemamu
Katibu Mkuu - JET
Machi 2, 2013
Tanbihi:
Viambatanisho
1. (Annex I) kinaonyesha mpango kazi (work
plan) wa JET kwa mwaka 2003
2. (Annex II) Rasimu ya bajeti ya fedha ya
JET 2013
No comments:
Post a Comment