MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, November 3, 2013

BONIFACE WAMBURA KAIMU KATIBU MKUU TFF

 
 Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Boniface Wambura.

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua  Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia Novemba 2 mwaka huu.

Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.

Kamati ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano  Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake.

Jamal Malinzi
Rais wa TFF
 Dar es Salaam
 Novemba 3, 2013

No comments:

Post a Comment