MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, March 23, 2012

Maonyesho ya Nguo za Harusi kufanyika Diamond Jublee Dar es Salaam



Ofisa Habari wa Fashion Show, Hamisa Juma akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na maonyesho ya mavazi yanayotarajia kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jublee hivi karibuni. katikati ni Hamis Omary na kulia ni mmoja wa washiriki wa maonnyesho hayo, Nicole Giannakopoulsou
 Moja kati ya Nyumba 53 zilizovunjwa katika Mtaa wa Lindi eneo la Kariakoo Dar es Salaam kupisha ujenzi wa Kituo cha Mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi jijini Dar es Salaam

Vitu vikiwa nje baada kuvunjwa Nyumba hizo
Hatujui twende wapi sasa maana nyumba zimebomolewa ndivyo walikuwa wakizungumza hawa akina mama baada ya nyumba zao kuvunjwa kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kasi

Bidhhaa za wafanyabiashara zikiwa zimeachwa wazi kufuatia kuvunjwa kwa vibanda kupisha ujenzi wa kituo cha mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi

Mabaki ya Nyumba eneo la Mtaa wa Lindi Dar es Salaam baada ya kubomolewa kupisha ujenzi wa Kituo cha mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi
Maisah mapya wapi sasa baada ya kuvunjiwa nyumba zao kupisha mradi wa Kituo cha Mabasi yaendyo kwa kasi
Baadhi ya wakazi waliokuwa wakiishi katika nyumba zilizovunjwa wakiwa hawana la kufanya baada ya kubomolewa nyumba zao

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng Ngosi Mwihava akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mkutano wa wadau Kupitia na kujadili Mwongozo wa ujumuishaji wa Masuala ya kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika Hotel ya Giraffe Ocean View Mjini Dar es Salaam


 


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng Ngosi Mwihava akizungumza na Mkugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais , Magdalena Mtenga wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa kutatua na kujadili Mwongozo wa Ujumuishaji wa Masuala ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Kwenye Hotel ya Giraffe Ocean View.

No comments:

Post a Comment