MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Friday, August 3, 2012

Maonyesho ya Nanenane Dodoma

Afisa Uhusiano wa Chuo cha Mipango Dodoma, Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha, Yulis Otto (kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo alioptembelea Banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Zuguni mjini Dodoma.
 

Kaimu Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF), Hawa Kikeke (kushoto) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko huo kwa watumishi wa umma (PSPF), Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia  Maafisa wa  Jeshi la Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Zuguni mjini Dodoma.
 

No comments:

Post a Comment