Jumla
ya warembo arobaini kati ya sitini wa Miss Utalii Tanzania kutoka mikoa yote ya
Tanzania.tayali wameripoti kambini leo,kuanza kambi Taifa ya siku 21 kuanzia leo. Kambi hiyo mwaka huu iko katika
Hoteli ya Ikondelelo Lodge iliyoko Kibamba Dar es Salaam.
Warembo
walio ripoti kambini hadi sasa ni kutoka mikoa ya Arusha (Rose Godwin), Dar es
Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine
Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob),
Kagera 1(Elline Bwire), Kagera2 (Jania
Abdul), Kagera 3(Mulky Uda), Kilimanjaro
(Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni),
Manyara (Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija
Said),Tanga (Sarafina Jackson), Tanga (Leah Makange), Tabora (Magreth Malalle),
Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha Ramadhani ),
Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma (Furaha Kinyunyu),
Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani (Beatrice Iddy), Singida
(Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu
(Hawa Nyange)
Warembo
wote wakiwa kambini,watapewa mafunzo na semina mbalimbali kuhusiana na Utalii,
Utamaduni, Uwekezaji, Afya ya Jamii, Elimu ya Jamii, Wanyama Pori, Mazingira,
Madini,Ulinzi Shirikishi n.k, chini ya jopo la wakufunzi la mashindano haya
wakiongozwa na mkufunzi mkuu (Chief Choreographer) Erasato Gideon, pamoja na Mkufunzi
Mkuu wa Ngoma za Asili Mariam A. Kweji toka Kaole Sanaa Group,Mkufunzi wa
Miziki na Dansi la Asuku Che Mundugwao,wakufunzi wa minato na miondoko ya
Urembo na Mitindo Caroline Y. Mrosso na Evamary Gamba .
No comments:
Post a Comment