Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa
taarifa ya kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
(TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku
wa kuamkia Jumatano Machi 6, 2013.
Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa
Absalom Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa
kulaaniwa na Watanzania wote.
CCM tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama
huo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na
kukomesha matukio ya namna hiyo.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la
Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda,
wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu
apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI
KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
No comments:
Post a Comment