Zimbabwe inapigia kura ya maoni kielelezo cha katiba
hii leo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi ufanyike nchini humo
uliokumbwa na utata mwaka wa 2008.
Hata hivyo malalamiko yametolewa kuwa huenda
nchi hio haijajiandaa vilivyo kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha na
wachunguzi wanadai kuwa wamefungiwa nje ya shughuli hiyo.
Lakini
kwa mara ya kwanza inaonekana kuwa hakuna kizungumkuti kikubwa katika
kura hii. Chama chake Rais Robert Mugabe ZANU - PF na kile cha upinzani
ambacho sasa kiko katika serikali ya muungano MDC, vyote vinaunga mkono
kielelezo hicho cha katiba.
Katiba hiyo inapendekeza kuhifadhiwa nafasi ya
rais mwenye nguvu nyingi serikalini na hii inampa rais Mugabe uwezo wa
kusalia madarakani kwa miaka kumi zaidi.
Hata hivyo kura hii ya maoni haijawachangamsha
sana wananchi wa Zimbabwe huku raia wengi wakionekana kulenga zaidi
uchagzui mkuu unaopangwa kufayika miezi chache zijazo.
Katiba mpya inatazamiwa kunyoosha njia ya
kufanyika uchaguzi huo mkuu japo kuna wasiwasi kwa machafuko zaidi
kutokea nchini humo.
No comments:
Post a Comment