Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la wahariri Neville Meena aliyeko Afrika Kusini katika Hospitali ya Mirlpak anakopata matibabu Kibanda
Wapendwa Wahariri,
Tupo katika hosiptali ya Milpark, Johannesburg
nchini Afrika Kusini kumjulia hali Mwenyekiti wetu, Absalom Kibanda ambaye kama
mnavyofahamu anapatiwa matibabu kutokana na tukio la kushambuliwa kwake.
Pamoja nami, pia wapo Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Jesse
Kwayu na Mhariri Mtenaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo.
Jana (Ijumaa) kutwa tulishinda naye hosipitalini
na kwa ujumla hali yake inaendelea kuimarika vizuri. Kama tulivyowaarifu tangu
juzi, ameanza mazoezi mepesi ya kusimama na kutembea na anaweza kukaa kwa muda
na kushiriki mazungumzo. Kwa hakika
amechangamka na anatia moyo.
Hata hivyo, bado mwenyekiti wetu
ataendelea kubakia hosipitalini kwa matibabu zaidi kama wanavyoshauri madaktari
wake. Jambo la msingi tuendelee
kumwombea katika sala zetu na wale ambao watapata fursa wafike kumjulia hali na
kumtia moyo.
Kwa muda tutakaokuwa hapa tutaendelea
kuwajulisha maendeleo ya afya yake. Pokeeni pia picha ambazo tumepiga tukiwa
pamoja naye hosipitalini akiwa ameketi kwenye kiti.
No comments:
Post a Comment