CHAMA cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimetangaza kuanza kwa Ligi Daraja
la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita bora.
Ofisa Habari wa
DRFA, Mohamed Mharizo, amesema hayo leo Aprili 5 kuwa ligi hiyo itaanza Aprili
9 mwaka huu hadi 31 katika viwanja vitatu vya Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Kinesi na Makurumla.
Alizitaja timu
zitakazochuana katika hatua hiyo kuwania kucheza Ligi ya Kanda Taifa kuwa ni
pamoja na Boom FC ya Ilala, Friends Rangers ya Magomeni, Abajalo FC ya Sinza,
Red Coast ya Mburahati, Day Break ya Magomeni na Shariff Star ya Ilala.
“Kwa mujibu wa
ratiba yetu, kila siku kutakuwa na mechi tatu, hivyo katika mechi za ufunguzi
Aprili 9, Boom FC wao watachuana na Shariff Star, kwenye Uwanja wa Airwing,
wakati Day Break watamenyana na Friends Rangers uwanja wa Makurumla huku Red
Coast wao watacheza dhidi ya Abajalo,” alisema Mharizo.
Timu tatu katika
ligi hiyo zitawakilisha mkoa katika Ligi ya Kanda Taifa hapo baadaye.
Wakati huo huo,
Mharizo amesema kabla ya kaunza kwa ligi hiyo, kutatolewa semina elekezi kwa
viongzi wa timu shiriki, itakayofanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Shule ya
BenjaminMkapa kuanzia saa nne asubuhi.
“Lengo la semina
hii elekezi ni kutoa elimu kwa viongozi na wachezaji ili kuondoa mvutano wakati
wa ligi hiyo, nia yetu ni nzuri na tunapenda kuona ligi ikichezwa kwa kufuata
kanuni na taratibu zilizowekwa,” alisema Mharizo.
Semina hiyo
itawahusisha Katibu, Mwenyekiti, Kocha, Nahodha na Waamuzi 16 watakaochezesha
ligi hiyo
No comments:
Post a Comment