Hatimaye kazi ngumu ya kutafuta miili iiyokuwa imefunikwa na kifusi kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 Dar es Salaam imekamilika ambapo imepatika miili ya watu 34 na kwa masikitiko makubwa pia vimepatika vichwa wiwili vikiwa havina viwiliwili,taarifa hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick wakati akitoa shukurani kwa watu wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika uwokoaji huo
Pichani juu hili ndilo shimo lililokuwa limewekwa msingi wa kubeba uzito wa ghorofa 16, hapo wanaonekana askari wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) na waokowaji wengine wakikusanya mchanga ndani ya shimo hilo ikiwa ni kuhitimisha kazi hiyo iliyochukuwa karibu siku nne
No comments:
Post a Comment