MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Monday, June 24, 2013

ZITTO AALIKWA KWENYE TAMASHA LA ASPEN IDEAS 2013

MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa
kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani.
Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali
duniani.
Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo
kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.
Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana
mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani.
Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo
litakaloendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika
katika sehemu mbili.
Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya
pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja.
Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa
nyanja mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.
Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto
na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa
zinazoikabili dunia hivi sasa.
Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na
waandishi wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata
fursa ya kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza.
“Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu
kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa
masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa
waalikwa mbali mbali. Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na
kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa
masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa kufafanua umuhimu wa
tamasha hilo kwa vijana.
Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na
Majaji washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na
Elena Kagan, Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan
Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene,
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi
ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza
wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani
Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans
Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa
zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican
Karl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.
TAAFIRA KWA WAHARIRI
KUHUSU TAASISI YA ASPEN
Taasisi ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina
makao makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni
kuendeleza maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha
kuwezesha kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.
Taasisi ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye
River huko Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi
ina mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.

No comments:

Post a Comment