CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) kimetuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Mjumbe wa Kamati ya
Nidhamu na Usuluhishi, Jimmy Mhango aliyefariki juzi katika hospitali ya
Muhimbili jijini Dar es Salaam kutokana na presha.
Katibu Mkuu wa DRFA Msanifu Kondo amesema leo
(Oktoba 22) kwamba wamepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mjumbe huyo,
ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji mahiri katika timu ya Ushirika ya Moshi katika
miaka ya tisini chini ya Kocha Dan Korosso.
Marehemu pia aliwahi kuzichezea timu za Pan Africans
ya Dar es Salaa pamoja na timu ya Mkoa wa Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Stars.
“DRFA imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Jimmy
Mhango na inatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na wanafamilia wote wa mpira wa
miguu, tunawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu,” alisema.
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya DRFA ambayo
marehemu alikuwa mjumbe, inaongozwa na Roman Masumbuko (Mwenyekiti), Fahadi
Kayuga (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Mpili (Mjumbe) na Peter Nkwera (Mjumbe).
Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo (Jumanne)katika makaburi ya
Ilala Mchikichini, Dar es Salaam saa kumi jioni.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema
Imetolewa
na Mohamed Mharizo
Ofisa
Habari
Chama Cha
Mpira Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
Oktoba 22,
2013
No comments:
Post a Comment