Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akizungumza na kutoa maagizo kwa Meneja wa
TRA Wilaya ya Bunda Mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo
kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Serikali mara alipotembelea ofisi ya TRA
Wilayani hapo ili kujionea namna ukusanyaji mapato unavyofanyika
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akimsisitizia jambo
Mfanyabiashara wa duka la nguo Wilayani Bunda mkoani Mara kuhusu suala la
umuhimu wa kutumia mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) mara
alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akikagua taarifa ya
mauzo ya siku ya Mashine ya Kielektroniki ya Kutolea Risiti (EFD) kutoka kwa
Wafanyabiashara wa duka la vifaa vya nyumbani wilayani Bunda mkoani Mara mara
alipofanya ukaguzi wa mashine hizo katika baadhi ya maduka
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TRA Wilaya ya Bunda mkoani Mara pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo mara alipotembelea ofisi ya TRA Wilayan. Picha zote na
BENEDICT LIWENGA-TRA
Na: Veronica Kazimoto,
Bunda,
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere
amemsimamisha kazi Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Nicodemus Mwakilembe kutokana na uzembe wa
kutosimamia vizuri matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti
(EFDs) kwa wafanyabiashara wa mkoani kwake.
Uamuzi huo umetokana na
ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya EFD aliyoifanya Kamshina Mkuu wa TRA
kwenye baadhi ya maduka ya biashara Wilayani Bunda Mkoa wa Mara.
Akizungumza mara baada ya
ziara yake, Kamishna Mkuu Kichere alisema Meneja huyo ameonyesha uzembe wa hali
ya juu kwani kuna wafanyabishara wengi mkoani kwake ambao walishalipa fedha kwa
ajili ya kupata mashine za EFD lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo.
"Katika ziara yangu
nimegundua kwamba, wapo wafanyabiashara ambao walikwisha kulipia mashine tangu
mwaka 2013, 2014 na 2015 lakini mpaka sasa bado hawajapatiwa mashine za EFD na
wamekuwa wakitumia mwanya huo kama kinga ya kutochukuliwa adhabu na TRA wakati
Meneja wa Mkoa yupo na hachukui hatua
zozote. Huu ni uzembe uliopitiliza na kamwe siwezi kuuvumilia," alisema
Kichere.
Kutokana na uzembe huo,
Kamishna Mkuu Kichere amewaagiza Mameneja wote wa TRA nchi nzima pamoja na
majukumu mengine, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mashine za EFD
katika mikoa yao na amesema hatasita kumuwajibisha Meneja yeyote atakayeshindwa
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Ziara hiyo ya kushtukiza imewawezesha
wafanyabiashara waliokuwa wamelipia mashine za EFD miaka ya nyuma, kupata mashine
hizo na kufundishwa jinsi ya kuzitumia ambapo wengine wamejitokeza kununua
mashine hizo kwa ajili ya biashara zao.
Kamishna Mkuu aliongeza
kuwa, mashine za EFD zina umuhimu sio tu kwa Serikali kupata mapato bali kwa
wafanyabiashara husika kwani huwawezesha kutunza kumbukumbu, kujua mwenendo
halisi wa biashara zao na hatimaye kulipa kodi stahiki.
Sambamba na hayo, Kichere
amewataka wananchi wasiishie tu kudai risiti bali wakishachukua risiti hizo
wazikague ili kuthibitisha uhalali wake na usahihi wa kiasi cha pesa
walicholipa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania yuko mkoani
Mara kwa ziara ya siku 5 ambapo amepata nafasi ya kutembelea Vituo vya Forodha
mipakani na ofisi mbalimbali za mamlaka hiyo pamoja na baadhi ya
wafanyabiashara akikagua matumizi ya mashine za EFD.
No comments:
Post a Comment