LIGI ya Wanawake Mkoa wa
Dar es Salaam inatarajiwa kaunza Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya
Benjamin Mkapa, Bandari na Makurumla.
Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo alisema kuwa ligi hiyo ni
moja ya mkakati wao wa kuimarisha mchezo ili uweze kuwa na hamasa kwa wanawake.
Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi
hiyo kuwa ni Mburahati Queens, Evergreen Queens, Sayari, Real Tanzanite, Uzuri
Queens, Simba Queens, BYC Queens, JKT Queens, Lulu
Queens, Mchangani Sisters, TMK Queens, Msimamo Queens na Mikocheni
Queens.
“Kwa kweli ligi ya wanawake nayo ni
muhimu kama ilivyo kwa wanaume, lengo letu ni kuona wanawake wanakuwa na ligi
yao na sisi tunaona hili ni jambo zuri ambalo litasaidia kupata wachezaji wa
timu ya taifa (Twiga Stars).
No comments:
Post a Comment