Aliyekuwa mgombe urais kupitia Chadema, Edward Lowassa akimsalimia, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad katika Hotel ya Serena , Dar es Salaam. Picha na Amanitanzania blog
Aliyekuwa mgombea urasi kupitia chama cha Chadema akiwakilisha UKAWA, katika Uchaguzi Mkuu 2015, Edward Lowassa leo amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad katika Hotel ya Serena, Dar es Salaam
Akizungumza baada ya kutembelewa na Lowassa Maali Seif Sharif Hamad alisema hali yake inazidi kuimarika na kwamba anaendelea vizuri kwa hiyo wananchi wasiwe na wasiwasi
Alipoulizwa na waandishi wa habari kama kuna chochote walichojadili kuhusu uchaguzi wa zanzibar alipotembelewa na Rais John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein yeye alisema hakuna walichozungumza kuhusu uchaguzi wa Zanzibar isipokuwa walikuja kumuona tu
No comments:
Post a Comment