Kamishna Generali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias
Andengenye akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam baada ya kupokea msaada
wa simu za mkononi kutoka Kampuni ya Airtel Tanzania
zitakazotumika kuimarisha mawasiliano ndani ya jeshi hilo kupitia
namba ya dharura 114.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano.
Kamishna Generali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias
Andengenye akipokea baadhi ya simu za mkononi ambazo zimetolewa na Airtel
Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kupitia namba ya dharura 114 ndani
ya jeshi hilo. Simu hizo zitasaidia wananchi wote kutoka mitandao yote
watakapopiga katika namba ya dharura 114 na kuhudumiwa kwa haraka. Habari na Picha kwa hisani ya Airtel Tanzania
Kampuni ya Airtel
Tanzania imekabidhi msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo
zitatumika kwa ajili ya kurahisisha na kuimarisha mawasiliano ya namba ya dharura
114 wakati wa kuripoti dharura za moto na majanga mbalimbali nchini.
Simu hizo zimetolewa
kwa mikoa maalumu ya Jeshi la Zimamoto ambapo wateja wa Airtel watapiga bure
ili kupata huduma za jeshi hilo.
Akikabidhi simu hizo,
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya alisema
wao kama Airtel wanatambua umuhimu wa Jeshi hilo na wanaamini kuwa wananchi
sasa wataweza kupata huduma za Jeshi hilo kwa urahisi kupitia namba hiyo ya
dharura.
“Airtel tunatambua
umuhimu wa jeshi la zimamoto na uokoaji katika jamii,hivyo tunaamini utoaji wa
taarifa za majanga kwa wakati muafaka unarahisisha shughuli za uokoaji na
kuzuia kwa kiwango kikubwa hasara ambayo inaweza kusababishwa na majanga hayo
katika jamii.
Alisema kupitia
namba hii ya dharura ya 114 na kwa uwezeshaji wa kuitumia kwa urahisi na
uhakika, Jeshi la Zimamoto litaweza kuwahudumia wananchi kwa haraka wakati wa
moto na majanga yanapotokea.
Alisema Airtel
itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo ili kuhakikisha mawasiliano yanafanyika
kwa urahisi na haraka ili kulisaidia jeshi la zima moto kuweza kuwafikia
wananchi wengi Zaidi kote nchini na kuepusha hasara zinazoweza kutokea wakati
wa majanga ya moto na kadhalika.
“Tunataka
kuwahakikishia wateja wetu wote kuwa mtandao wa Airtel uko imara kwa kuwa hivi
karibuni tumeboresha zaidi mtandao kwa kutumia teknolojia mpya ya U900 katika
baadhi ya mikoa ikiwemo hii inayofaidika na huduma ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, hivyo basi tunawaomba muitumie namba hiyo ya dharura vizuri huku pia
mkifaidi huduma zetu bora za Airtel ,” alisema.
Mikoa iliyopokea simu
hizo ni pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke, Pwani, Morogoro, Dodoma, Iringa,
Mbeya, Songwe, Njombe, Mwanza, Mara, Shinyanga, Tabora, Simiyu, Geita, Kagera,
Katavi, Kigoma, Rukwa, Ruvuma, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Mtwara,
Lindi, Singida na Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment