TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKABIDHI MSAADA WA MAFUTA YA KUZUIA MIONZI YA JUA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) TANZANIA YAMEKABIDHIWA SIKU YA WALEMAVU DUNIANI Jumamosi, Tarehe 03 Desemba, 2011, Dar Es Salaam, Tanzania Shirika lisilo la kiserikali la Hands of Africa Foundation lenye makao makuu yake mjini Dan Bosch nchini Uholanzi lenye tawi hapa Tanzania ambalo ni Hands of Africa Foundation(Tanzania) lina ofisi zake jijini Dar Es Salaam, Manispaa ya Ilala, Kata ya Tabata Mtaa wa Mandela, linalojishughulisha na kutoa huduma na misaada mbalimbali ya kijamii na elimu ya afya kwa jamii hususani kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), leo linakabidhi msaada wa chupa elfu moja (1,000) za mafuta ya kuzuia mionzi ya jua kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) hapa Tanzania. Msaada huo wenye mafuta kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) una thamani ya shilingi 25,000,000/= (milioni ishirini na tano) umetolewa na shirika rafiki la AmeriCares la Stamford la nchini Marekani. Watakaonufaika na msaada huo ni watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wa Dar Es Salaam wa kutoka mkoa mbalimbali. Walengwa wapatao mia tano (500) watanufaika na msaada huo kwa kila mmoja kupata chupa mbili ya mafuta hayo kila moja ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi elfu ishirini na tano (25,000/=) katika soko la Tanzania. Shirika la Hands of Africa Foundation Tanzania limetoa msaada huo kwa kutambua kuwa idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa Tanzania hawana uwezo wa kununua mafuta hayo ya kuwakinga na mionzi ya jua ambayo ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya saratani ya ngozi. Wito kwa serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi kuunga mkono juhudi za shirika la Handa of Africa Foundation Tanzania katika kuwasaidia na kuwahudumia ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Pongezi za dhati ziwafikie ndugu Francis Chibunda Mfamasia na uongozi mzima wa Bugando Hospitali kwa kuwezesha mafuta haya kutufikia..na wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha mchakato mzima
Taarifa hii imetolewa na : Joseph Sinda Mratibu wa Mpango Hands of Africa Foundation Tanzania, S.L.P. 62849, Simu - + 255 713 212 428
|
No comments:
Post a Comment