MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, April 15, 2012

Rais Jakaya Kikwete ziarani nchini Braziri kikazi

 Mke wa Rais Mama Salma kikwete akipokea shada la maua mara baada ya yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili  katika Hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kulia kwake ni Rais Kikwete na nyuma kulia ni  Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman na mwenye miwani ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Francis Malambugi

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Raymond Mbilinyi,   baada ya kuwasili katika Hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na mwandishi mwandamizi wa Habari Leo na Daily News,Joseph Lugendo, alipokuwa analakiwa baada ya kuwasilii   Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo

 Rais Jakaya Mrisho kikwete na Mama Salma Kikwete  wakiwasili Jumapili Aprili 15, 2012 katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo, Brazil, tayari kwa ziara ya siku tano ya kikazi nchini humo. Kulia ni  Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar ,Haroun Ali Suleiman
Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongea na Msaidizi Mwandamizi wa Rais (Diplomasia) Balozi Liberata Mulamula baada ya Mkutano wa maandalizi ya ziara yake ya siku tano nchini Brazil Jumapili Aprili 15, 2012 katika Hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo. katikati  ni  Waziri wa kazi na Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun Ali Suleiman.

No comments:

Post a Comment