HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO (MB), WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI, KUHUSU MAPENDEKEZO YA
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
______________________
I. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, ninatoa
maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Bajeti ya Nchi ya mwaka wa fedha 2012/2013
kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(7) toleo la Mwaka 2007.
Mheshimiwa Spika, Natoa pongezi za dhati
kabisa kwa Ndugu William Augustao Mgimwa, Mbunge wa Jimbo la Kalenga mkoani
Iringa kwa kuteuliwa na Rais kuwa Waziri wa Fedha na Uchumi. Vile vile
nawapongeza Ndugu Saada Mkuya na Ndugu Janeth Mbene kwa kuteuliwa kwao kuwa
Wabunge na baadaye kuwa Manaibu Mawaziri katika Wizara hii nyeti sana. Ninawapa pole pia maana Wizara ya Fedha sio
Wizara lelemama. Kambi ya Upinzani itaendelea kuisimamia Wizara hii kwa ukaribu
sana kama ilivyofanya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Mtakapofanya
vizuri tutawapongeza ili muongeze juhudi, mtakapoharibu tutawawajibisha.
Mheshimiwa Spika, Ni dhahiri kwamba Mwaka
wa Fedha uliopita ulikuwa mwaka mgumu sana kwa Watanzania. Ni mwaka ambao
gharama za maisha zilipanda kwa kasi kubwa sana
na juhudi za Serikali
kuwakwamua wananchi na hasa wananchi wanyonge kutoka kwenye lindi la ufukara
ziligonga mwamba. Kambi ya Upinzani inawapa pole Watanzania kwani hili ndilo
walilochagua. Muhimu ni kuvumilia mpaka uchaguzi ujao na kufanya mabadiliko ya
Serikali ili kuweka Serikali itakayoongozwa na CHADEMA na itakayoweza kukabili
changamoto za sasa na za baadaye.
Mheshimiwa
Spika, naomba tufanye mapitio kidogo ya Bajeti inayomaliza muda wake.
- UTEKELEZAJI WA BAJETI ILIYOPITA
Mheshimiwa
Spika, kabla ya kutoa
bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani ni vema kufanya tathmini ya utekelezaji wa
bajeti ya Serikali iliyopita ili kuona ni kwa namna gani Serikali inathamini
fedha za walipa kodi, na dhamira yake ya kuleta maendeleo ya kiuchumi katika
Taifa. Katika kufanya hivyo, tutapitia baadhi ya maeneo ambayo Kambi ya Upinzani
tunaona kuwa hayakutekelezwa katika bajeti iliyopita.
Kupunguza Makali ya Maisha
Mheshimiwa Spika, Katika Bajeti ya mwaka 2011/12 Serikali ilitangaza nia yake ya
kupunguza makali ya maisha. Hatua mbali mbali zilichukuliwa ikiwamo kupunguza
kodi na tozo kwenye mafuta ya Dizeli na Petroli, kuanza kutekeleza mpango wa
dharura wa umeme na kutoa fedha za kununua chakula kwa Wakala wa Chakula. Serikali ilitumia shilingi
bilioni 296 na dola za Marekani milioni 183 kwenye Umeme. Vilevile Serikali
ilitumia shilingi bilioni 27 kununua Mahindi na kusambaza kwenye masoko.
Mheshimiwa Spika, licha ya hatua hizo zilizochukuliwa Mfumuko wa Bei
uliongezeka maradufu kutoka wastani wa asilimia 6.3 mwaka 2010/11 mpaka wastani
wa asilimia 17.8 mwaka 2011/12. Serikali imefeli katika lengo lake la kupunguza
makali ya maisha kwa wananchi. Sio tu kwamba Serikali imeshindwa kudhibiti
upandaji holela wa gharama za maisha bali pia hatua za Serikali zimeongeza kasi
ya kupanda kwa makali ya maisha.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni katika Hotuba yake mbadala ya mwaka 2011/12 iliitaka
Serikali kushughulikia msingi wa mfumuko
wa Bei hapa nchini ambao ni uzalishaji mdogo wa mazao ya chakula. Tumeelezwa na
Waziri Kivuli wa Mipango na Uchumi kwamba Chakula peke yake ni asilimia 48 ya
kapu la bidhaa na huduma ambazo mwanachi anatumia. Mfumuko wa Bei ya Chakula
kinacholiwa nyumbani na kwenye migahawa ilikuwa asilimia 25 mwezi Aprili 2012
(BoT monthly Economic Review, May 2012). Vile vile mfumuko wa bei wa nishati
inayotumika nyumbani na mafuta ya Dizeli na Petroli ulifikia asilimia 25 pia
mwezi Mei mwaka 2012. Ni dhahiri kwamba iwapo tutadhibiti mfumuko wa bei ya
chakula tutaweza kushusha mfumuko wa bei kurudi kwenye tarakimu moja.
Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza hatua zilezile ilizofanya mwaka wa fedha
unaokwisha kwa kutoa vibali kwa Wafanyabiashara vya kuagiza Mchele na Sukari.
Katika hotuba yake Waziri wa Fedha anasema ‘….Serikali ilitoa vibali vya kuagiza sukari bila kutoza ushuru wa forodha
kiasi cha tani 200,000 ili kukabiliana na uhaba na kupanda kwa bei ya Sukari…’(uk
9 ibara ya 15). Baada ya hatua hii bei ya Sukari ilipanda kutoka tshs 1700
mpaka tshs 2800 kwenye maeneo mengi nchini. Waziri wa Fedha katika hotuba yake
anatoa suluhisho. Ninanukuu. ‘…hatua za haraka ambazo Serikali itachukua ni
pamoja na kutoa vibali vya uagizaji wa Sukari na mchele kutoka nje….’! Serikali
inachukua hatua zilezile kwa tatizo lile lile ikitegemea matokeo tofauti.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inarejea pendekezo lake la mwaka jana kwa
Serikali kutoa vivutio kwa wakulima wadogo kuzalisha chakula kwa wingi.
Miongoni mwa vivutio hivyo ni:
i.
Kuwekeza
kwenye barabara za vijijini ili mazao yao yafike kwenye masoko na kupata bei
nzuri,
ii.
Kuwekeza
kwenye Usambazaji wa Maji vijijini ili kina mama wasitembee mwendo mrefu
kutafuta maji na hivyo kutumia muda mwingi kwenye uzalishaji,
iii.
Kuwekeza
kwenye Umeme vijijini ili wafanyabiashara wa vijijini waongeze thamani ya mazao. Kwa mfano, kuuza Unga badala ya Mahindi.
iv.
Kuwekeza
kwenye miundombinu ya Umwagiliaji vijijini ili wakulima wazalishe muda wote wa
mwaka.
v.
Kuwekeza
kwenye Elimu vijijini na pia Afya vijijini ili wananchi wetu wawe na Afya bora
na waelimike katika mbinu za uzalishaji bora.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaamini kuwa, hakuna mbadala wa kudhibiti mfumuko
wa bei zaidi ya kuongeza uzalishaji wa chakula na kuwekeza kwa wananchi wetu.
Serikali inafikiria uzalishaji utaongezeka kwa kusaidia wakulima wakubwa ambao
watageuza wananchi wetu kuwa Manamba na vibarua ndani ya nchi yao. Tuwekeze kwa
watu wetu vijijini ili waongeze uzalishaji na kwa kufanya hivyo mfumuko wa Bei ya chakula utakuwa historia. Hakuna mwarobaini wa kupanda kwa bei za vyakula
isipokuwa Kilimo.
Mhesimiwa Spika, Tunatambua kuwa hatua tunazotaka Serikali ifanye ni za muda wa kati.
Kwa muda mfupi tunataka Bodi ya Mazao mchanganyiko, Wakala wa Hifadhi ya
Chakula na Bodi ya Sukari zipewe fedha kuagiza Mchele na Sukari na pia kununua
kutoka kwa wakulima na kusagisha Mahindi. Wafanyabiashara waagizaji wa Chakula
washindane na Taasisi hizi za Umma badala ya kuwapa vibali ambavyo hutolewa kwa
rushwa na hivyo kuongeza bei za bidhaa hizo.
Kuwezesha Wananchi Kiuchumi na Kuongeza Ajira.
Mheshimiwa Spika, Serikali imesema kwamba ilichukua hatua mbalimbali kukabiliana na
tatizo la Ajira kwa kuongeza fursa za ajira. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa
ni pamoja na kuongeza mitaji katika Benki ya Rasilimali, Benki ya Wanawake,
Benki ya Posta na Twiga Bancorp. Pia Serikali imetangaza kwamba imeajiri
walimu, maafisa ugani na watumishi wa Afya. Hatua kama hizi pia zimetangazwa
kwa mwaka wa Fedha wa 2012/13 ambapo pia Serikali imetangaza kuajiri watumishi
71,756.
Mheshimiwa Spika, Duniani kote Serikali haizalishi ajira bali ajira huzalishwa na Uchumi
mzima ambapo Serikali ni sehemu tu ya Uchumi (Jobs are created by the economy). Takwimu zinaonyesha kwamba kila
mwaka Tanzania inaingiza kwenye soko la Ajira watu takribani laki saba.
Shughuli za Uchumi zikiongezeka ndio Ajira zinatengenezwa. Serikali inafikiria nini
kuhusu vijana takribani milioni nane walio shule za Msingi hivi sasa, Vijana
milioni 1.7 walio katika Shule za Sekondari hivi sasa, Vijana 200,000 waliopo
vyuo vya Ufundi na Wanachuo 180,000 walio katika Vyuo vya Elimu ya Juu (takwimu
kutoka kitabu cha hali ya uchumi, 2012 sura ya 19). Serikali ambayo bado
inategemea takwimu za Ajira za Mwaka 2006 inajitamba kwa kuajiri watu 70,000.
Mheshimiwa Spika, Jukumu la Serikali ni kujenga mazingira ya wananchi kupata ajira ama
kwa kujiajiri au kwa kuajiriwa na shughuli za uchumi. Lakini ukweli ni kwamba Serikali
imeshindwa kushughulikia tatizo la Ajira na hasa ajira kwa vijana. Tatizo la
Ajira kwa Vijana ni Bomu litakalokuja kutulipukia vibaya sana kama hatutakuwa
makini nalo. Hii ni nchi ya Vijana. Kutoshughulikia masuala yao ni
kutoshughulikia masuala ya nchi.
Mheshimiwa Spika, changamoto ya ajira kwa vijana Bajeti mbadala imeiwekea mikakati
mipana ya kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa ya Umma itakayomeza vijana
waliopo mtaani na kuanzisha kwa makusudi na kwa kasi Vyuo vya Ufundi stadi na
Vyuo vya Ufundi na Mafunzo vingi. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza
Uwekezaji wa Miundombinu Vijijini kama njia ya kupunguza tatizo la ajira kwa
vijana. Vilevile tunapendekeza Miradi mikubwa ya kuongeza mazao ya Kilimo hasa
Pamba, Korosho na Katani ili kupanua Ajira. Kambi ya Upinzani pia inapendekeza
kujenga VETA katika kila Halmashauri ya Wilaya na Chuo cha Ufundi katika kila
Mkoa ili kutoa ujuzi kwa vijana ili waweze kukabili maisha yao. Badala ya
Serikali kukopa kwa ajili ya Matumizi ya kawaida, Serikali ikope kujenga Vyuo
vya Ufundi Stadi na vyuo vya Ufundi na Mafunzo. Ni Lazima viongozi sio tu tuwe
makini bali tuonekane kuwa makini tunaposhughulikia suala la Ajira kwa Vijana.
Sera ya Mapato
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza vipaumbele
katika sera ya Mapato ambavyo ni pamoja na kukusanya Mapato ya Serikali mpaka
zaidi ya asilimia 20 ya Pato la Taifa ili kuwezesha kujitegemea kupata fedha za
miradi ya maendeleo. Pia Kambi ya Upinzani inakusudia kufanya marekebisho
mbalimbali ya sheria za kodi ili kulinda viwanda vya ndani vinavyotumia
malighafi za kilimo na mifugo za hapa nchini, kupanua wigo wa Mapato kwa
kutunga sheria ya kulazimu kila Mtanzania kujaza fomu za marejesho ya kodi na
kurekebisha viwango vya kodi ya Mapato (PAYE). Vile vile tunapendekeza kufanya
marekebisho ya sheria za kodi kwenye sekta za madini na mawasiliano ili
kuongeza mapato ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa Fedha 2011/12 Serikali ilichukua hatua mbalimbali
katika masuala ya Kodi. Katika Bajeti mbadala pia tulipendekeza hatua mbali
mbali ambazo tuliona zitaongeza mapato ya Serikali na hivyo kutuwezesha
kuendeleza nchi yetu. Baadhi ya hatua mbalimbali tulizopendekeza Serikali
imetangaza kuzitekeleza.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
katika Bajeti Mbadala ya mwaka 2011/12 ilipendekeza masuala yafutayo ili
kuongeza mapato ya Serikali.
- Hatua zifuatazo zilipendekezwa ili kuweza
kukabiliana na ukwepaji wa kodi unaofanywa na makampuni makubwa ya
kimataifa (Multinational Corporations) na hatimaye kulipunguzia taifa
mapato:
(i)
Kutunga
sheria kwa kuimarisha zaidi sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 kwamba,
mikopo ya makampuni kwenye uwekezaji, kwa sababu za kikodi, isizidi asilimia 70
ya mtaji wote uliowekezwa na hii ianze mara moja bila kujali mikataba iliyopo.
(ii)
Kutunga
sheria kuhakikisha kwamba riba kwenye mikopo kutoka Makampuni yanayohusiana
(sister companies) haitaondolewa kwenye kutoza kodi (not tax deductible).
(iii)
Kuhakikisha
kwamba mauziano ya Kampuni yoyote ambayo mali zake zipo Tanzania yanatozwa kodi
ya asilimia 30% kama ‘ongezeko la mtaji’ (‘capital gains’).
Mheshimiwa
Spika, katika mapendezo
haya ni pendekezo moja tu ndilo limechukuliwa na Serikali katika Bajeti ya
mwaka 2012/13 nalo ni pendekezo la ‘capital gains tax’. Hata hivyo Pendekezo la
Serikali lina makosa makubwa sana ya kifundi. Waziri wa Fedha Mhe. Mgimwa
amesema, ninanukuu ‘Kuanzisha kodi itokanayo na uuzaji wa rasilimali ya
uwekezaji (capital gains tax) kwenye uuzaji wa HISA za kampuni mama ya nje ya
nchi’
Mheshimiwa
Spika, Ukisoma pendekezo
letu kwa haraka utaona kama Serikali imelichukua lilivyo, lakini kwa jicho la
kiuchumi pendekezo la Serikali na lile la Kambi ya Upinzani ni mambo tofauti
sana. Pendekezo la Serikali linazungumzia HISA. Mamlaka ya Mapato Tanzania
haitakuwa na mamlaka (jurisdiction to tax) kutoza kodi kwa Kampuni mama (as a
source or even residence). Mamlaka ya Mapato Tanzania ina mamlaka na Mali
(assets) zilizopo Tanzania za Kampuni mama. Kwa mfano, wakati kampuni ya
Barrick inanunua mgodi wa Bulyanhulu haikuinunua Kampuni ya Kahama mining ltd
bali ilinunua hisa zote za Kampuni ya Sutton Resources. Vile vile, wakati Zain
inanunua Celtel, haikununua Celtel Tanzania ltd bali Celtel Africa BV ambayo
ilikuwa inamiliki Celtel Tanzania BV ambayo ilimiliki Celtel Tanzania ltd.
Hivyo hivyo ilikuwa kwa AirTel ilipoinunua Zain. Kukwepa mitego hii ya Mashirika ya Kimataifa (MNCs) sheria itaje kwamba
Kodi hii itozwe kwa Mali zilizopo Tanzania na sio kwa HISA kama alivyopendekeza
Waziri wa Fedha. Hata hivyo Kambi ya Upinzani inatambua hatua hiyo ya
Serikali kuchukua wazo hili ili kuongeza Mapato ya nchi.
Misamaha
ya Kodi
Mheshimiwa
Spika, Katika Bajeti ya
mwaka 2011/12 Serikali iliahidi kupunguza misamaha ya Kodi mpaka kufikia
asilimia 1 ya Pato la Taifa. Ahadi hii haikutekelezwa na Serikali na badala
yake imerejea kuahidi tena. Waziri wa Fedha ameliambia Bunge katika hotuba
yake, nanukuu ‘kuendelea kufanya mapitio
ya sharia mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodi kwa lengo la kudhibiti na
kupunguza misamaha hiyo’ (uk.39). Badala ya Serikali kutuambia hivi sasa
misamaha ya kodi imefikia asilimia ngapi, imeendelea kutoa ahadi isizoweza
kutekeleza.
Mheshimiwa
Spika, Katika Taarifa ya
Utafiti uliofanywa na Jopo la Taasisi za dini hapa nchini waliyoiita ‘The One Billion Dollar Question’ imeonekana kwamba Tanzania
inapoteza takribani shilingi trilioni 1.7 kutokana na misamaha ya kodi,
ukwepaji wa kodi, utoroshaji wa mitaji nje na udanganyifu katika biashara ya
kimataifa. Fedha hizi ni zaidi ya jumla ya Bajeti za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Nishati na Madini. Fedha hizi ni zaidi ya Mkopo ambao Serikali itadhamini
kwa TPDC ili kujenga Bomba la Gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. Fedha
hizi zinazopotea kutokana na misamaha ya kodi ni zaidi ya gharama za Ujenzi wa
Gati mpya katika Bandari ya Dar es Salaam. Kambi ya Upinzani inawapongeza
Viongozi wa Dini kwa kufanya kazi hii nyeti sana lakini tunampongeza zaidi
Mtafiti Mtanzania Dokta Prosper Ngowi kwa kushiriki katika utafiti huu.
Tunaishauri Serikali kusoma Taarifa hii na kutekeleza mapendekezo yake ili
kuongeza mapato ya Serikali. Lugha za kufanya mapitio kila mwaka hazisaidii,
wananchi wanataka kuona misamaha ya kodi imepungua mpaka kiwango kinachostahili
cha asilimia 1 ya Pato la Taifa.
Kurekebisha
mfumo wa Kodi ya Mapato
Mheshimiwa
Spika, Bajeti mbadala ya
mwaka 2011/12 ilipendekeza kuifanyia marekebisho sheria ya Kodi ya Mapato ya
mwaka 2004. Tunarejea pendekezo letu na kuongeza pia kwamba sehemu ya kodi ya
Mapato inayotoa fursa (grandfathering) kwa Kampuni za Madini kutumia sheria ya
kodi ya Mapato iliyofutwa ya mwaka 1973, ifutwe. Pendekezo letu lina lengo la
kutaka kuweka mfumo wa ‘straightline method of depreciation’ ya asilimia 20
badala ya sasa ambapo Kampuni za Madini hufanya ‘100% depreciation’ kwenye
Mitambo yao mwaka wa kwanza na hivyo kuchelewesha kulipa ‘Corporate Tax’.
Mheshimiwa
Spika, Serikali imeamua
kupandisha kiwango cha chini cha kipato ili kutoza kodi ya Mapato (PAYE) kutoka
tshs 135,000 mpaka tshs 170,000 bila kushusha kodi yenyewe. Hii haitamsaidia
mwananchi hata kidogo kwani bado kiwango cha kodi cha asilimia 14 kipo juu sana. Vile vile
kiwango cha chini cha pato litakalotozwa kodi kitawaathiri wafanyakazi wa
Serikali maana ndio ambao Serikali ina mamlaka ya kutangaza kima cha chini cha
Mshahara wao na kuwaacha wafanyakazi wa Sekta Binafsi ambao wengi hulipwa
kiwango kidogo sana cha mishahara. Kimsingi kutokana na tangazo lake, Waziri wa
Fedha ametangaza kima kipya cha chini cha mshahara kuwa kitakua tshs 170,000.
Mheshimiwa
Spika, tunarejea kauli
yetu kwamba kupanda kwa gharama za maisha kumepunguza uwezo wa matumizi ya
wananchi walioajiriwa na kulipwa mishahara ambayo inakatwa kodi (PAYE). Tunapendekeza
kwamba PAYE ianzie asilimia 9 kutoka asilimia 14 na kiwango cha chini cha
kutoza kiwe tshs 150,000. Tunatambua kuwa kodi hii ni chanzo kikubwa cha Mapato
kwa Serikali ambapo kwa mwaka huu wa Fedha kinatarajiwa kuingiza takribani
shilingi bilioni 1,437 (asilimia 18 ya Mapato yote ya kodi yanayokusanywa na
TRA) kutoka Idara ya Kodi za Ndani (Wafanyakazi wa Serikali tshs 115bn,
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma tshs 47bn na Wafanyakazi wa Sekta binafsi tshs
312bn) na Idara ya Walipa kodi wakubwa (Wafanyakazi wa Serikali tshs 450bn,
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma Tshs108bn na Wafanyakazi wa Sekta Binafsi tshs
406bn). Hata hivyo wananchi wanapobakia na pesa za matumizi kodi nyingine kama
VAT na Ushuru wa Bidhaa huongezeka na hivyo kupunguza kiwango cha Mapato ya
Serikali ambayo yangepotea kutokana na uamuzi huu.
Mheshimiwa
Spika, Hata hivyo bado kuna
haja ya kuangalia upya ‘tax brackets’
na kuzirahisisha kwa kuzipunguza na kuongeza kiwango cha kodi ya Mapato kwa
watu wenye kipato kikubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika, ili kuongeza mapato kutoka kwa watu wenye kipato kikubwa kambi
ya Upinzani inapendekeza mabadiliko katika viwango vya juu vya kodi ya Mapato
ambapo tunapendekeza kupandisha kiwango cha juu kabisa cha kukokotoa kodi ya
mapato (PAYE) kiwe shilingi milioni kumi na kodi iwe asilimia 42 kutoka
asilimia 30 ya sasa.
Mheshimiwa Spika, Tunapendekeza kwamba mtu yeyote anayepata mapato ya zaidi ya
shilingi 10,000,000 alipe kodi ya Mapato ya shilingi 500,000 kujumlisha na
asilimia 42 ya tofauti ya shilingi 10,000,000 na shilingi 3,200,000 kama
inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini. Lengo la mapendekezo haya ni kuwafanya
watu wenye kipato kikubwa walipe kodi zaidi kulingana na kipato wanachopata
maana hivi sasa masikini wanalipa kodi nyingi zaidi kuliko wenye nacho.
|
Mapato
ya kutozwa kodi kwa mwezi
|
Kodi (PAYE)
|
Mapendekezo
ya mapato ya kutozwa kodi kwa mwezi
|
Kiwango kipya cha Kodi (PAYE)
|
|
Mapato
yanayozidi shilingi 720,000
|
Sh. 112,500
ongeza 30% ya kiasi kinachozidi sh. 720,000
|
Mapato yanayozidi 720,000 lakini hayazidi sh. 3,199,199
|
Sh.112,500 ongeza 30% ya ziada ya sh. 720,000
|
|
|
|
Mapato yanayozidi sh. 3,200,000 lakini hayazidi
sh.9,999,999
|
Sh.190,000 ongeza 38% ya ziada ya 3,200,000.
|
|
|
|
Mapato kuanzia sh. 10,000,000 na kuendelea
|
Sh. 500,000 ongeza 42% ya mapato yake.
|
Mheshimiwa
Spika, Mapendekezo haya
hayatapunguza Mapato ya Serikali kwani wigo wa kodi utakuwa umeongezeka kwa
kuwagusa wafanyakazi katika sekta binafsi na pia kupata kodi zaidi kutoka kwa
watu wenye kipato kikubwa zaidi.
Mheshimiwa
Spika, vile vile Kambi ya
Upinzani inaendelea kupendekeza kuwa mchakato uanze ili kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na zaidi awe anajaza fomu za kodi
(tax returns) kila mwaka. Suala hili ni muhimu sana na litangazwe mwaka huu
ili tuwe na mwaka mzima wa kujitayarisha ili lianze Mwezi Julai mwaka 2013. Mtanzania
yeyote, awe na kipato au asiwe na kipato ajaze Tax Returns. Mfumo huu utatoa
takwimu muhimu sana kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania na utasaidia sana hapo
baadaye kupanua wigo wa Mapato. Tunapendekeza marekebisho katika Sheria ya Kodi
ya Mapato ili mfumo huu uwepo kisheria ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.
Mheshimiwa
Spika, Vile vile, Kambi ya
Upinzani inapendekeza kuanzishwa kwa Real
Estate Regulatory Authority kama tulivyofanya kwa mwaka uliopita na kwamba
kila mwenye nyumba ya kupangisha lazima atambuliwe na kulipa kodi inavyostahili.
Lengo ni kuhakikisha Sekta ya Nyumba inatoa mapato ya kutosha kwa Serikali na
kuzuia mianya ya ukwepaji kodi inayofanywa na wenye nyumba.
Presumptive
Tax
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
Bungeni ilipendekeza mwaka 2011/12 kwamba ushauri wa Mradi wa kuboresha mfumo
wa kodi (Tax Modernisation Project) ambao ulishauri kwamba ipo haja ya
kuainisha Kodi ya VAT na Presumptive Tax, utekelezwe. Tunashauri kuwa kodi
anayotozwa mfanyabiashara ndogondogo kabla hajaanza kufanya biashara ifutwe
kabisa. Uamuzi huu utapunguza mapato ya Serikali (Shilingi bilioni 21.6 kwa
mujibu wa Kitabu cha Bajeti Vol. I) katika kipindi cha muda mfupi lakini
itakuwa ni chanzo kikubwa sana cha mapato katika kipindi cha muda mrefu.
Vyanzo vipya vya Mapato
Mheshimiwa
Spika, Pamoja na kupitia vyanzo vya mwaka jana na kulinganisha na
mapendekezo ya Serikali, Kambi ya Upinzani bado inapendekeza vyanzo vya ziada
mwaka huu ili kuboresha Mapato ya Serikali.
Kupanua
wigo wa Skills Development levy
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
tunapenda kushukuru kuwa wazo letu la kutoza kodi ya skills development levy tuliyopendekeza katika hotuba yetu ya mwaka
uliopita lilifanyiwa kazi na serikali lakini kwa mwaka ujao wa fedha tunaitaka
serikali kuipitia upya kodi kwa kuongeza wigo wa wachangiaji ili kuwa na fedha
za kutosha kwa ajili ya kugharamia elimu ya juu.
Mheshimiwa
Spika, tunapendekeza
kiwango cha tozo ya kuendeleza stadi (skills
development levy – SDL) kishuke kutoka asilimia 6 ya sasa mpaka asilimia 4.
Tunapendekeza kuwa Waajiri wote walipe kodi hii ikiwemo Serikali na Mashirika
ya Umma. Lengo ni kupunguza mzigo kwa Waajiri na kuondoa ubaguzi kwani
wanaofaidika na tozo hii (wanafunzi wa elimu ya Juu) pia huajiriwa na Serikali
na Mashirika ya Umma. Serikali ilipanga kukusanya tshs 161bn kutoka katika tozo
hii kwa mfumo wa sasa.
Mheshimiwa
Spika, Marekebisho ambayo
Kambi ya Upinzani inayapendekeza yataongeza mapato ya Serikali mpaka tshs
320bn.
Mheshimiwa
Spika, Waziri wa Fedha
katika tozo hii amesema Serikali ‘itapitia upya maudhui ya viwango vya tozo’
hii. Kambi ya Upinzani imetamka maudhui na viwango na tunaiomba Serikali
itekeleze pendekezo hili.
Mheshimiwa
Spika, Tunapendekeza
mgawanyo wa tozo hii urekebishwe kwa kuongeza mapato yatakayokwenda kwenye Vyuo
vya Ufundi mchundo.
Mheshimiwa
Spika, kama wanafunzi wetu
watasomeshwa na kodi hii basi tuangalie upya mfumo wa Mikopo ya wanafunzi wa
Elimu ya Juu. Fedha inayopatikana kwenye Kodi hii itumike kusomesha kwa ‘grant’
wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi darasani na kuwapunguzia mzigo wa mikopo.
Vile vile tuangalie kama tunaweza kukopesha wanafunzi malazi na chakula tu na
kutoa bure ada na mafunzo kwa vitendo pamoja na vitabu.
Kulinda
kazi za Wasanii
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
mara kwa mara tumekuwa tukieleza jinsi wasanii wanavyoshindwa kunufaika na kazi
zao kutokana na kukosekana mfumo rasmi wa kiserikali unaozuia wizi wa kazi za
wasanii. Pamoja na serikali kukubali kuahidi kuwa na mfumo rasmi wa kuzuia wizi
wa kazi hizo, serikali haijaweka wazi mfumo rasmi utakaokuwa unatumika kuzuia
wizi huo na hatimaye wasanii kunufaika na kazi zao.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya upinzani
katika hotuba ya Wizara ya Habari Vijana na Michezo kwa mwaka uliopita
tulingumzia suala hili na tulishauri kwamba kuwe na utaratibu wa kuweka sticker maalumu zinazotolewa na mamlaka
za serikali kuonyesha uhalali wa muuzaji wa kazi za wasanii. Serikali
imetekeleza pendekezo letu. Hata hivyo tuna maoni tofauti kuhusu namna ya
kutekeleza pendekezo hili.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa
kumbukumbu zilizopo, serikali mwaka 2006 kupitia gazeti la Serikali Na. 18 la
tarehe 10 Mwezi wa Februari, ilianzisha utaratibu wa HAKIGRAM kama stiker
maalumu za kazi halali za wasanii zinazotolewa na COSOTA. Kambi ya Upinzani
tunapendekeza utaratibu huo uendelee na Mamlaka ya Mapato TRA ihusike kukusanya
mapato kwa ajili ya kazi hiyo na COSOTA wataratibu utoaji wa HAKIGRAM. Hii
itaenda sambasamba na kuzuia uchakachuaji wa HAKIGRAM hizo ili kutopoteza lengo
la kuweka mfumo huo. Stiker zisitolewe na TRA bali zitolewe na COSOTA na TRA
isimamie eneo la Mapato tu. Hii itasaidia kwani stiker hizi hazitatumika kupata
mapato peke yake bali pia kuweka kumbukumbu muhimu za kazi za wasanii.
Mapato
kutoka Sekta ndogo ya Mawasiliano ya Simu
Mheshimiwa
Spika, serikali imekuja na
pendekezo la kuendelea na kutoza ushuru wa bidhaa kwenye masuala ya huduma ya
mawasiliano ya simu, jambo ambalo litamgusa mtumiaji wa huduma hiyo ambaye ni
mwananchi wa kawaida na hivyo kuongeza gharama za simu. Kambi ya Upinzani
inapinga kabisa kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye muda wa Maongezi (airtime)
kwenye simu za mkononi.
Mheshimiwa
Spika, Hoja ya wananchi
hapa ni kwamba Kampuni za Simu za mkononi hazilipi kodi ya kutosha na hasa kodi
ya Makampuni (corporate tax). Waziri Mkuu alipokuwa anafunga Bunge la Bajeti
mwaka 2011 alitangaza Kampuni ambazo ni walipa kodi wakubwa katika kipindi cha
miaka 5 iliyopita. Katika orodha hiyo kulikuwa na Kampuni moja tu ya Simu za
Mkononi (Kampuni ya AirTel).
Mheshimiwa
Spika, wakati wananchi
wanataka kodi zaidi kutoka Kampuni za simu, Serikali inapendekeza kuongeza kodi
kwa mwananchi anayetumia simu. Kampuni zilipe kodi ya Mapato na sio kukandamiza
wateja kwa ushuru wa bidhaa ilihali huduma zenyewe za simu hazina ubora.
Mheshimiwa
Spika, vilevile wananchi
wanalalamika kwamba Kampuni za simu za Mkononi hajiweki wazi mapato yake yote
hali iliyopelekea Kamati ya Bunge ya POAC kuiagiza TCRA kufunga mtambo
utakaoweza kuijulisha TCRA mapato yote ambayo kampuni za Simu zinapata.
Serikali ya Ghana ilifanya hivi na kupandisha maradufu mapato yanayotokana na
sekta ndogo ya simu. Hivi sasa Ghana, nchi yenye watumiaji wa simu milioni 17
ukilinganisha na Tanzania yenye watumiaji 23 milioni, inakusanya asilimia 10 ya
Mapato ya Serikali kutoka kwenye kampuni za Simu peke yake. Iwapo Tanzania
ikifikia kiwango cha Ghana cha asilimia 10 ya Mapato ya ndani ya Serikali
kutoka kwenye kampuni za simu, Tanzania itaweza kukusanya zaidi ya Shilingi
bilioni 860 kutoka kwenye sekta ndogo ya simu peke yake. Hata hivyo mazingira
ya Ghana na Tanzania ni tofauti na hivyo tunapendekeza kiwango kutokana na hali
yetu.
Mheshimiwa
Spika, Shirika la TCRA
kupitia zabuni nambari AE-020/2010-11/C/04 imetangaza ‘request for expression of interest for design, development,
installation and Management of Telecommunication monitoring system under build,
operate and transfer’ ili kupata chombo cha kufuatilia Mapato ya Kampuni za
Simu. Kwa mujibu wa ratiba zilizotangazwa na TCRA chombo kitakuwa kimeanza kazi
mwishoni mwaka huu wa 2012. Kwa dhati kabisa napenda kumpongeza Mkurugenzi Mkuu
wa TCRA na watumishi wote kwa kutekeleza maelekezo ya Kamati ya Bunge kwa
haraka ili kuhakikisha mapato kwa nchi yetu.
Mheshimiwa
Spika, kilichotushangaza ni
kwamba Waziri wa Fedha na Uchumi hakugusia kabisa suala hili muhimu sana kwa
mapato ya Serikali badala yake Serikali imekimbilia kukandamiza wanyonge
watumiaji wa Simu na kuyaacha Makampuni ya Simu yakilipa kiduchu kutoka kwenye
mapato yao.
Mheshimiwa
Spika, uamuzi huu wa
kufuatilia mapato ya Kampuni za Simu na Marekebisho tunayopendekeza ya kujenga
uwezo zaidi wa TCRA kwa kuwa na Idara ya ‘Revenue Assurance’ na kurekebisha sheria
ya TCRA kwa kuweka wazi makujumu ya TRA ndani ya TCRA, utaiingizia Serikali
mapato ya takribani tshs 660bn.
Mheshimiwa
Spika, katika eneo hili la
Sekta ya Mawasiliano ninaomba kurejea kuitaka Wizara ya Fedha itoe maelezo hapa
Bungeni namna ambavyo Hisa za serikali katika Kampuni ya MIC Tanzania ltd
inayomiliki Kampuni ya Tigo zilivyouzwa. Mheshimiwa Spika Serikali ilikuwa inamiliki hisa
asilimia 26 katika Kampuni hii. Kwa mujibu wa kumbukumbu nilizoziona Hisa hizi
zote ziliuzwa kwa thamani ya dola laki saba kwa mwana hisa mwenza mnamo mwezi
Februari mwaka 2004. Kampuni hii leo inapata mapato ya Tshs bilioni 20 kwa
mwezi, tuliuza hisa zetu asilimia 26 kwa dola laki saba! Laki Saba dola! Kambi
ya Upinzani inataka uchunguzi maalumu katika mauzo haya na Taifa liambiwe nini
kilitokea na hatua gani za kuchukua
dhidi ya waliouza mali hii ya Umma bila zabuni wala kuzingatia thamani ya
fedha.
Kuzuia mauzo ya ngozi ghafi nje ya nchi
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani imeshangazwa
na hatua ya serikali kuja na pendekezo la kuongeza ushuru kwenye bidhaa ya
ngozi ghafi inayosafirishwa nje kutoka asilimia 40 hadi 90 lengo likiwa ni
kuhamasisha usindikaji wa ngozi hiyo na kuiongezea thamani.
Mheshimiwa Spika, kwa nchi iliyo na mianya
mingi ya rushwa kama Tanzania hatua hii haitakuwa na tija kwa kuwa
wafanyabiashara wengi wa ngozi ghafi wamekuwa na tabia ya kupunguza takwimu za
kusafirisha ngozi ghafi na hivyo kupelekea serikali kukosa mapato mengi sana.
Serikali inafahamu kwamba hata ushuru wa mauzo nje wa asilimia 40 haukuweza
kutatua tatizo la viwanda vya ndani kukosa malighafi. Kambi ya Upinzani
haikubaliani na Pendekezo la Serikali kwani halitatatua tatizo la kukuza sekta
ndogo ya Ngozi nchini.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani tunaitaka
serikali kuzuia kabisa kusafirisha ngozi ghafi kwenda nje na badala yake kuwe
na mpango wa kutumia ngozi ghafi hapa nchini na kuleta tija katika uchumi wa
taifa kwa kutengeneza ajira na kuongeza thamani ya mauzo nje.
Mheshimiwa Spika, hatua ya kuzuia ngozi ghafi
kusafirishwa kwenda nje kwa Tanzania itakuwa sio suala jipya kwa sababu
Ethiopia imezuia na kuwekeza katika kiwanda cha viatu, mikanda na bidhaa za
ngozi. Kutokana na Mpango wa Mendeleo ya Ethiopia (GTP – Growth and
Transformation Plan) sekta ya Ngozi itaingiza fedha za kigeni za thamani ya
dola za Kimarekani bilioni 4 kwa mwaka. Hii ni sawa na fedha za kigeni ambazo
Tanzania inapata kutoka kwenye Dhahabu na Utalii kwa pamoja. Ethiopia nchi
iliyokuwa inatembea na bakuli na kulia njaa leo inakuwa nchi ya kupigiwa mfano
na sisi Watanzania! Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda pia amepiga marufuku
kuuza ngozi ghafi nje. Hata nchi ya Pakistani ambayo ndio ngozi zetu zinakwenda
nayo imepiga marufuku mauzo ya ngozi ghafi nje. Serikali ipige marufuku Mauzo
ya ngozi ghafi nje ya Nchi ili kulinda viwanda vya ngozi nchini, kuoongeza
Ajira na kuongeza mapato ya Fedha za kigeni.
Kufuta Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa bidhaa
za Maziwa
Mheshimiwa Spika, sekta ndogo
ya Maziwa hapa nchini inahitaji kuwekewa maazingira ya kukua ili izalishe ajira
na mapato ya kodi kwa Serikali. Wakati Tanzania ndio nchi ya Afrika Mashariki
inayoongoza kwa kuwa na Ng’ombe wengi lakini inaongoza kwa kuagiza maziwa
kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani 3.6m. Wakati Kenya imelinda soko
la Maziwa na Bidhaa za Maziwa kwa kuondoa (zero rating) kodi ya VAT kwenye
bidhaa za Maziwa, Waziri wa Fedha hajaonyesha kabisa juhudi zozote za kujengea
uwezo sekta ndogo ya Maziwa hapa nchini na hivyo kuweza kuondolewa kabisa
katika ushindani na kujikuta wafugaji wanakosa kabisa soko la kuuza maziwa yao
hapa nchini. Nchi za Rwanda na Uganda pia zimelinda Maziwa na Bidhaa za maziwa
kwa njia hii. Ni muhimu Serikali kuwianisha kodi hii na Nchi nyingine za Afrika
Mashariki.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani
inapendekeza kufanya marekebisho kwenye sharia ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
kwa kufanya ‘zero rating’ kwenye Maziwa na Bidhaa za Maziwa zinazozalishwa hapa
nchini kwa kipindi cha miaka 5 ili kufikisha uzalishaji wa angalau lita 500,000
za maziwa kwa siku kutoka lita 123,000 za sasa na kuweza kutoa ajira kwa
watanzania zaidi ya elfu tatu.
Mheshimiwa Spika, hatua zote za kuongeza
mapato tulizopendekeza pamoja na hatua za Bajeti Mbadala iliyopita ambazo
tunarudia kuzipendekeza zitaongeza Mapato ya Serikali kwa takribani shilingi
bilioni 2,885 kama inavyoonyeshwa katika jedwali hapa chini.
NYONGEZA YA VYANZO VYA MAPATO MBADALA 2012/2013
|
Chanzo cha Mapato
|
Makisio - Bilioni
|
|
Marekebisho ya kodi za misitu ikiwemo Mkaa
|
130.8
|
|
Kupunguza misamaha ya kodi, kuzuia ukwepaji kodi na udanganyifu wa
Biashara ya Nje
|
742.74
|
|
Mauzo ya hisa za serikali
|
415.55
|
|
Marekebisho ya kodi Sekta ya
madini (kodi ya Mapato, Kodi ya CGT na ushuru mbalimbali) (25% ya Mauzo
ya Madini Nje)
|
578.36
|
|
Marekebisho ya Kodi na Usimamizi bora wa Mapato Kampuni za Simu
|
502.26
|
|
Marekebisho
ya Kodi ya SDL
|
243.52
|
|
Mapato ya wanyamapori
|
61.64
|
|
Kuondoa msamaha wa ushuru wa mafuta- kampuni za madini
|
44.9
|
|
Usimamizi wa mapato ya utalii
|
51.75
|
|
Kuimarisha biashara katika EAC kwa kuongeza mauzo
|
114.15
|
|
JUMLA
|
2,885.67
|
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema hapo juu, vyanzo hivi vya mapato ni mjumuisho wa
vyanzo ambavyo katika hotuba zetu mbadala za nyuma tumekuwa tukipendekeza,
ambapo tumevifanyia marekebisho kulingana na hali halisi ya uchumi ulivyo kwa
sasa, pamoja na kupendekeza baadhi ya marekebisho ya sheria za kodi ili
kuongeza mapato zaidi kwa Serikali.
DENI
LA TAIFA
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
inasikitika kwa serikali kuendelea kutengeneza madeni kwa Taifa kwa kuendelea
kukopa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya serikali. Wakati Serikali inasisitiza
kwamba Deni letu linastahmilika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali
anaonyesha mashaka makubwa sana kutokana na kasi ya kukua kwa Deni la Taifa.
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kuongezeka kwa
asilimia 38 kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka 2009/2010 hadi shilingi
trillion 14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Deni la Taifa
limefikia shilingi trillion 20.3 mpaka ilipofika mwezi Machi mwaka 2012.
Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa
sasa limefikia shilingi trillion 22.
Mheshimiwa
Spika, Suala hapa sio
ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikali bali ni kwamba tunakopa kufanyia
nini? Bajeti ya Mwaka 2012/13 inayopendekezwa inaonyesha kwamba Serikali
itakusanya shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi
trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida. Ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo
ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida. Hatutaki
mikopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue
mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi.
Bajeti inaonyesha kwamba Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka
2012/13. Serikali ikubali kutekeleza mapendekezo ya Kambi ya Upinzani ya kuimarisha ukusanyaji wa
kodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama sekta ya madini na
mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza ukwepaji kodi, na kuepuka
matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
inapenda kusisitiza kwamba Bunge lifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Deni
la Taifa ili kuweza kubaini ukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na mikopo ambayo
Serikali inachukua kama inakwenda kwenye Maendeleo na miradi ipi na kama miradi
hiyo ina tija. Vilevile tumependekeza kwamba Mikopo yote ambayo Serikali inachukua
iwe inapata idhini ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge
sharia ili kiwango cha juu cha kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. Kuiacha
Serikali inaendelea kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupeleka
mzigo wa kulipa madeni haya kwa kizazi kijacho. Hatuwezi kukubali Wazee wetu waishi maisha yao, waishi maisha yetu na
pia wakope maisha ya watoto wetu.
Mheshimiwa Spika, Ukiangali sura ya Bajeti ya Serikali, inaonyesha kuwa Serikali
itakopa fedha zenye masharti ya kibiashara ndani na nje yenye thamani ya Tshs. Trilioni 2.89 kwa
kipindi hiki cha 2012/13. Athari ya
mikopo ya kibiashara ya ndani ni kubwa
sana kwa watanzania, kwanza inawafanya wananchi hasa wajasiriamali wanaokopa
kushindana na Serikali yao,
kwani mabenki yatashindwa kuwakopesha wafanyabiashara au wakikopa watakopa kwa
masharti magumu na hasa riba kuwa kubwa. Jambo hili linapunguza uwezo wa
wazalishaji kuongeza uzalishaji hasa viwandani kwa kukosa mikopo ya uendeshaji.
Kama tulivyoshauri hapo juu, Serikali ijiepushe na mikopo ya masharti ya
kibiashara kwa kuongeza makusanyo ya kodi.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya Serikali kuwa imepata Mshauri
Mwelekezi atakayeishauri katika kujiandaa kufanyiwa tathmini ya uwezo wa kukopa
na kulipa madeni. Serikali ilieleze
Bunge ni lini na kwa namna gani zabuni ya kumpata mshauri huyu ilitangazwa na
kama Sheria ya Manunuzi ilifuatwa.
Mwenendo wa Matumizi.
Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15
trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13 kama ilivyowasilishwa na Waziri
wa Fedha na Uchumi wiki iliyopita. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha
kwamba mafungu ya juu 5 yatakayoongoza kwa matumizi kwenye Bajeti hiyo ni Kama
ifuatavyo;
1. Huduma
kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni (USD 1.69 Billion)
2. Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4. Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5. Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
Jumla TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
2. Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3. Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4. Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5. Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
Jumla TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge
Mheshimiwa Spika, Jumla
ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti yote, kwa hiyo asilimia 40%
ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu na kati ya hayo Wizara ni nne tu za
Ujenzi, Elimu, Ulinzi na Nishati na Madini. Wizara ya Kilimo wala Afya hazimo
kabisa katika Wizara 5 zitakazopata fedha nyingi zaidi katika Bajeti. Fungu
lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo
kwa Deni la Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati
ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miaka ya nyuma. Shilingi
bilioni 40 ambazo zimetengwa kwa ajili ya Mradi wa Kiwira katika Wizara ya
Nishati na Madini ni kwa ajili ya kulipia Madeni ya Kampuni ya TanPower
Resources ambayo iliuziwa Mgodi wa Kiwira na kushindwa kuundeleza.
Mheshimiwa Spika, Madhara ya Deni la Taifa yanaonekana hapa katika
matuumizi ya Serikali ambapo tunapokuwa tunalipa madeni tunachukuwa rasilimali fedha nyingi kutoka kwenye Miradi ya Maendeleo.
Wakati Bajeti ya Maendeleo ni shilingi trilioni 4.5, Bajeti ya kugharamia Deni
la Taifa ni shilingi trilioni 2.7 (sawa na nusu ya Bajeti nzima ya Maendeleo).
Mheshimiwa Spika, Bajeti ya 2012/13 ni ya kulipa madeni zaidi kuliko
Bajeti ya kuchochea maendeleo ya Taifa letu. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni
Bajeti ya kukopa zaidi maana jumla ya TZS 5.1 trilioni (USD 3.19 Billion)
zitachukuliwa na Serikali kama mikopo
kutoka vyanzo mbalimbali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana
itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita.
Mheshimiwa Spika, Mgawanyo wa rasilimali za nchi kwenye sekta za kipaumbele (Miundombinu
ya usafirishaji kama reli, bandari, ndege viwanja vya ndege n.k), Barabara,
nishati,kilimo na mifugo, ili kuinua uchumi zimetengewa fedha kidogo sana kuweza
kuleta tija kulingana na malengo ya Mpango wa Maendeleo kama ulivyopitishwa na
Bunge lako tukufu. Bajeti iliyotengwa kwa ajili ya nishati imeshuka kwa kiwango
cha shilingi 40 bilioni, pia kwa mwaka uliopita fedha zilizotengwa kwa ajili ya
miundombinu,reli na TEHAMA zilitengwa shilingi 2,781.4 bilioni kwa 2011/12 ikilinganishwa na shilingi 1,505.1
bilioni kwa mwaka 2010/2011,(hili lilikuwa ni ongezeko la asilimia 85). Kwa bajeti
ya mwaka huu inaonesha sekta zilezile za
vipaumbele; bajeti iliyotengwa ni shilingi 1.394.5 bilion ambayo ni pungufu ya
asilimia 49.86 kwa kulinganisha na mwaka 2011/2013.
Mheshimiwa Spika,
wakati Waziri wa Fedha analiambia Bunge kuwa ametenga shilingi bilioni 1,383
kwa ajili ya Usafirishaji na Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi imetengewa shilingi
bilioni 1,000 kati ya hizo. Wizara ya Uchukuzi yenye Reli, Bandari, Viwanja vya
Ndege na Usafiri wa Maziwa ya Tanganyika, Nyasa na Viktoria imetengewa chini ya
shilingi bilioni 380. Serikali pia haijasema fedha ambazo zilitengwa na Bunge
katika Bajeti inayomaliza muda wake na kuzielekeza kwenye Wizara ya Miundombinu
na Wizara ya Uchukuzi zimetumikaje maana bado wakandarasi wanadai na fedha za
Reli hazikutoka zote kama ilivyopitishwa na Bunge.
Mheshimiwa Spika, wizara
nyingi hazikupata fedha za Maendeleo kama zilivyopitishwa na Bunge. Halmashauri
za Wilaya ndio zilipata hali mbaya zaidi katika kupata fedha za Maendeleo
ambapo kwa wastani ni asilimia 47 tu ya Bajeti ndio ilipelekwa katika
Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa. Kutokana na hali hii Wabunge kama
wawakilishi wa wananchi walihoji Serikali kwenye Kamati zao na kupata majibu
ambayo sio ya kuridhisha hivyo kupelekea Wabunge kugomea baadhi ya Wizara.
Mheshimiwa Spika,
Ushahidi wa hayo ni baadhi ya Kamati za
Kudumu za Bunge kukataa kukubali Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa baadhi ya
Wizara zilizo chini ya Kamati hizo. Wizara ambazo hazikupitishiwa /Kukubaliwa
makadirio yake ni pamoja na;
·
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
·
Wizara ya Uchukuzi, na (nilishangaa kumwona Waziri wa Uchukuzi akiwaahidi
wananchi pale Jangwani kwamba Reli inakarabatiwa vya kutosha ilhali Kamati
haijapitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara yake kwa kuwa haikupewa fedha za
kutosha)
·
Wizara ya Kilimo, Chakula
na Ushirika
Mheshimiwa Spika, kabla
Bunge lako tukufu halijajadili Makadirio ya Matumizi ya mwaka unaokuja ni vema Serikali itueleze kwanza fedha zilizotengwa
mwaka uliopita na hazikufika hatima yake nini?
Mheshimiwa Spika, uwiano wa bajeti iliyotengwa kwa matumizi ya kawaida
ambayo ni asilimia 70% wakati bajeti ya maendeleo asilimia 30% haiwezeshi nchi
kupiga hatua ya haraka ya Maendeleo. Kama ilivyoonyeshwa na Waziri Kivuli
Mipango na nitakavyohitimisha hotuba hii, Serikali imetayarisha Bajeti hii bila
kuzingatia masharti yaliyowekwa na Mpango wa Maendeleo uliopitishwa na Bunge
kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ibara ya 63 (3)(c) kwa kutotenga asilimia 35
ya Mapato ya ndani ya Serikali kwenye Bajeti ya Maendeleo.
Mheshimiwa
Spika, Serikali imekuwa ikitenga
fedha kidogo katika miradi ya maendeleo katika bajeti zake. Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), matumizi ya kawaida ya Serikali yanaongezeka huku
matumizi katika shughuli za maendeleo yanapungua mwaka hadi mwaka. Takwimu katika jedwali hapa chini zinaonyesha
|
Fungu
|
2009/2010
|
%
|
2010/2011
|
%
|
|
Fedha
za matumizi ya kawaida (Sh)
|
6,251,629,581,428
|
73
|
7,587,424,923,903
|
77
|
|
Fedha
za matumizi ya maendeleo (Sh)
|
2,299,010,652,135
|
27
|
2,223,684,150,465
|
23
|
|
Jumla
|
8,550,640,233,563
|
100
|
9,811,109,074,368
|
100
|
Chanzo: Ripoti ya CAG, uk. 21
Aidha, kwa miaka miwili iliyopita yaani 2009/2010
na 2010/2011 kumekuwa hakuna uwiano wa fedha za Maendeleo kama bajeti
zilivyopitishwa na Bunge dhidi ya fedha zinazotolewa na hazina kwa ajili ya
maendeleo katika Wizara na Idara. Tazama jedwali;
|
Mwaka
|
Bajeti
iliyoidhinishwa
|
Fedha
halisi zilizotolewa
|
Tofauti
(Sh)
|
%
|
|
2009/2010
|
2,825,431,400,000
|
2,299,010,652,135
|
526,420,747,865
|
19
|
|
2010/2011
|
3,750,684,569,000
|
2,223,684,150,465
|
1,527,000,418,535
|
41
|
Chanzo: Ripoti ya CAG, uk.22
Mheshimiwa
Spika, Kutokana na
takwimu hizi, jumla ya Sh.
1,527,000,418,535 au asilimia 41 ya fedha zilizoidhinishwa kwa maendeleo
hazikutolewa katika mwaka wa fedha 2010/2011, na kiasi cha Sh.
526,420,747,865 au asilimia 19 ya fedha
zilizoidhinishwa mwaka 2009/2010 hazikutolewa pia. Hii ina maana kuwa shughuli
za maendeleo za kiasi hicho cha fedha hazikutekelezwa kwa miaka husika.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
inatafsiri hali hiyo kama utovu mkubwa wa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma
kwa upande wa Serikali, Vilivile inaonesha ni jinsi gani Serikali yetu
haithamini maendeleo ndio maana kila mwaka Serikali inazidisha matumizi yake na
kuhakikisha kuwa inayapata kwa wakati huku ikipunguza bajeti ya maendeleo na
kutotoa fedha zote kama zilivyoidhinishwa na mbaya zaidi hata zile zinazotolewa
hazitolewi kwa wakati muafaka. Hii inafanya kukaa hapa Dodoma na kupitisha
Bajeti kuwe hakuna maana maana Bajeti haitekelezwi kama ilivyopitishwa.
Mheshimiwa
Spika, Kiasi kinachotengwa
kwa ajili ya maendeleo kimeshuka kutoka shilingi trilioni 4.9 katika mwaka wa
fedha 2011/12 hadi kufikia kiasi cha
shilingi trililioni 4.5 mwaka huu wa fedha 2012/13. Pamoja na serikali kushindwa kutekeleza
miradi ya maendeleo katika bajeti iliyopita, bado imeendelea kupunguza bajeti ya maendeleo katika bajeti
hii. Ni dhahiri serikali haizingatii
swala la maendeleo ya mwananchi, pia kutoona njia ya kuweka mkazo katika
maendeleo na kuendelea kupuuzia maazimio ya mpango wa maendeleo wa miaka
mitano.
Mheshimiwa
Spika, katika Bajeti
mbadala, Kambi ya Upinzani imetenga asilimia 36.06 na kukidhi matakwa ya Mpango
wa Maendeleo ya Taifa kutoka katika mapato ya ndani kwa matumizi ya maendeleo
kama Mpango wa Maendeleo ya Taifa ulivyoelekeza.
Mheshimiwa
Spika, Tuliamua kama Taifa
kwamba Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano ndio safina yetu ya kuelekea nchi ya
ahadi (middle income country). Mpango ukapitishwa na Bunge na kuwekwa sahihi na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inasikitisha kuona kuwa Serikali
inatoboa kisiri siri safina hii wakati tupo kati kati ya maji! Ninaamini
wananchi wanawaona wanaotoboa safina yetu na watawatosa kabla hawajazamisha
Taifa zima kwa kushindwa kutekeleza Mpango unavyoelekeza.
Ubadhirifu
wa fedha zinazotengwa
Mheshimiwa
Spika, pamoja na fedha za
maendeleo kutolewa kidogo kulinganisha na bajeti inayopitishwa na Bunge, bado
kumekuwepo na matumizi yasiyo na tija na ubadhirifu mkubwa.
Mheshimiwa Spika, upotevu wa fedha za umma umeendelea
kuwa kikwazo
kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi. Uchambuzi wetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2010/2011 pekee, umebaini takribani jumla ya Bilioni 12.9 (12,968,168,985) za fedha za umma zimepotea kama ongezeko kutoka shilingi billion 11.9 (11,152,048,065) ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ya upotevu wa fedha za Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010,hii inaonyesha kuwa Serikali inaona ni jambo la kawaida kupoteza viwango hivi vya pesa za Serikali na kambi ya upinzani kuwasisistiza wananchi kuendelea kuitathmini Serikali yao sasa ili kuweza kufanya maamuzi sahihi dhidi ya Serikali yao.
kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi. Uchambuzi wetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2010/2011 pekee, umebaini takribani jumla ya Bilioni 12.9 (12,968,168,985) za fedha za umma zimepotea kama ongezeko kutoka shilingi billion 11.9 (11,152,048,065) ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ya upotevu wa fedha za Serikali kwa mwaka wa fedha 2009/2010,hii inaonyesha kuwa Serikali inaona ni jambo la kawaida kupoteza viwango hivi vya pesa za Serikali na kambi ya upinzani kuwasisistiza wananchi kuendelea kuitathmini Serikali yao sasa ili kuweza kufanya maamuzi sahihi dhidi ya Serikali yao.
MAPENDEKEZO
YA KAMBI YA UPINZANI
SERA YA MATUMIZI 2012/13 KWA
BAJETI MBADALA
Mheshimiwa Spika,
lengo kuu la Bajeti Mbadala ni kuhakikisha uchumi unakua katika maeneo ya
vijijini kwa kati ya asilimia 6 na 8 ili kuleta Maendeleo ya wananchi na
kutokomeza umasikini. Kwa njia hiyo ni
dhahiri wananchi wapatao milioni 30 waishio vijijini watanufaika na matumizi ya
raslimali zao.
Vipaumbele vya bajeti ya
Matumizi.
(i)
Kujenga Mazingira ya Ukuaji wa
uchumi vijijini (rural growth) kwa kuboresha miundombinu ya umeme, barabara,
maji na miundombinu ya Umwagiliaji. Tunapendekeza kutumia shilingi bilioni 600
kila mwaka (bilioni 150 kwa kila sekta niliyotaja). Fedha hizi zitasimamiwa na
Mamlaka ya Maendeleo Vijijini (Rural Development Authority – to be established)
itakayokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
(ii)
Kukarabati Reli ya Kati na matawi
yake ya Tanga/Arusha na Mpanda. Tutatenga tshs 443bn kwa RAHCO kwa ajili ya
Reli. Lengo ni kuhakikisha Reli ya Kati inafikia uwezo wa kusafirisha Tani 1.5m
kwa mwaka na hivyo kulipatia Taifa fedha za kigeni katika sekta ya usafirishaji
kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Tunataka sekta ya usafirishaji iliingizie
Taifa fedha za kigeni mpaka dola za kimarekani 1.5 bilioni kutoka dola 0.5
bilioni za sasa.
(iii)
Kuboresha Elimu na Afya hasa kwa
Shule na Zahanati/Vituo vya Afya vya Vijijini kwa kutoa motisha kwa wafanyakazi
wa Sekta hizi walio kwenye Halmashauri za Wilaya. Tunapendekeza posho za
Mazingira ya Vijijini kwa Walimu, Madaktari na Manesi sawa na mara moja na nusu
ya Mishahara yao. Vile vile tutaongeza mishahara ya Walimu, Manesi na Madaktari
kwa asilimia 50, pamoja na kuboresha stahili zingine za kazi ili kuvutia
Watanzania wengi zaidi katika maeneo haya na kuboresha huduma zao kwa wananchi.
(iv)
Kuongeza Kima cha chini cha Mshahara
kwa Wafanyakazi wa Umma mpaka Tshs 315,000 kwa Mwezi
(v)
Kuanzisha Pensheni ya uzeeni kwa
Wazee wote nchini wenye umri wa zaidi ya miaka 60.
(vi)
Kujenga Uwezo wa Viwanda vya ndani
ili Kuuza nje bidhaa za kilimo na mifugo zilizoongezewa thamani. Tutazuia kuuza
nje Korosho ghafi na Ngozi ghafi kwa kuanzia. Lengo ni kufufua viwanda vyote
vya nguo na kuanzisha viwanda vipya kwa kutoa motisha kwa wawekezaji
watakaotumia malighafi za hapa nchini.
(vii)
Kupunguza mzigo wa matumizi ya
magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi’ na kuweka mfumo wa
kukopesha Magari kwa watumishi wote wa Umma wanaostahili Magari kama alivyofanya
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. Katika Taarifa yake kwa Kamati ya Fedha na
Uchumi, Waziri wa Fedha alitamka, ‘….kufanya mapitio ya stahili za aina za
magari kwa viongozi wa ngazi
mbalimbali na kuandaa mwongozo wa kugharamia ununuzi wa vyombo vya usafiri ili
kupunguza matumizi ya magari, mafuta na matengenezo ya magari…’ kama hatua za
kubana matumizi. Hatua hii ya kupunguza gharama za magari Waziri hakuisema
kabisa katika hotuba yake Bungeni.
(viii)
Kuendelea kusisitiza kufutwa kwa
posho za vikao katika mfumo mzima wa malipo na stahili kwa watumishi wa Umma.
Katika Taarifa yake kwa Kamati ya Fedha, Waziri wa Fedha alitamka ‘…. Kufanya
mapitio ya posho na stahili zote kwa lengo la kuziwianisha….’ Suala hili nalo
Waziri hakulizungumza kabisa katika Hotuba yake Bungeni.
(ix)
Kuanzisha Chuo Kikuu cha Mtwara
(Mtwara University for Petroleum Studies) ili kuzalisha wataalamu wa kutosha wa
Sekta ya Mafuta na Gesi na kuliandaa Taifa kuwa na wasomi mahiri wa maeneo hayo
na hivyo kufaidika na Utajiri wa Mafuta na Gesi uliopo nchini kwetu.
Tunapendekeza shilingi bilioni 200 mwaka huu katika Bajeti ya Wizara ya Elimu
kwa ajiri ya Mradi huu.
(x)
Kutunga sheria mpya ya Mashirika ya
Umma (Public
Corporations
Act)
ili kujengea uwezo Ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vyema Mashirika yote ya Umma
ambayo Serikali inamiliki kwa zaidi ya asilimia 100 na kutoa nguvu za kisheria
kwa Shirika la CHC kuweza kusimamia hisa za Serikali katika Kampuni na
Mashirika ambayo Serikali
inamiliki chini ya asilimia 50.
(xi)
Kupunguza gharama za safari za nje
kwa kupunguza ukubwa wa misafara na madaraja ya kusafiria. Eneo hili la safari
za nje limekuwa likiigharimu Serikali fedha nyingi sana.
Mheshimiwa Spika,
kufuatia hatua mbali mbali za kikodi tulizozichukua Kambi ya Upinzani
inapendekeza Bajeti ya shilingi trilioni 15 ambazo zitapatikana kwa Mapato ya
ndani ya shilingi trilioni 11.9 na misaada na mikopo ya kibajeti ya shilingi
trilioni 3.2 kama ilivyopendekezwa na Serikali. Kambi ya Upinzani inapendekeza
Serikali kutokukopa kibiashara ili kudhibiti ukuaji wa Deni la Taifa.
Mheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba Serikali itatumia shilingi
trilioni 9 katika Matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 6 kama Matumizi ya
Maendeleo. Katika fedha za Maendeleo, asilimia 35 ya Mapato ya ndani
yameelekezwa huko kama ilivyoagizwa na Mpango wa Maendeleo ya Taifa
ulioidhinishwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba.
SURA YA BAJETI MBADALA YA MWAKA
2012/2013
|
|
MAPATO
|
SHILINGI
MILIONI
|
|
|
A
|
Mapato ya ndani
|
|
11,889,078
|
|
|
i)mapato ya kodi (TRA)
|
|
|
|
|
ii)Mapato
yasiyo ya kodi
|
|
|
|
B
|
Mapato
ya Halmashauri
|
|
|
|
C
|
Mikopo
na Misaada ya kibajeti (GBS)
|
842,487
|
|
|
D
|
Misaada
na mikopo ya miradi ya maendeleo nay a kisekta
|
2,314,231
|
|
|
|
i)Misaada
|
1,465,461
|
|
|
|
ii)Misaada na mikopo
kisekta
|
415,137
|
|
|
|
iii)MCC(MCA-T)
|
433,634
|
|
|
|
Jumla ya Misaada na mikopo ya kibajeti
|
|
3,156,718
|
|
|
|
|
|
|
|
JUMLA YA MAPATO
YOTE.
|
|
15,045,796
|
|
|
MATUMIZI
|
|
|
|
E
|
Matumizi ya
Kawaida
|
|
9,000,000
|
|
H
|
Matumizi ya
Maendeleo
|
|
|
|
|
(i)Fedha
za ndani
|
4,161,177
|
|
|
|
(ii)Fedha
za Nje
|
1,884,619
|
|
|
|
Jumla ya matumizi
ya maendeleo
|
|
6,045,796
|
|
|
JUMLA YA MATUMIZI
YOTE.
|
|
15,045,796
|
Hitimisho
Fedha
za Rada
Mheshimiwa
Spika, Wakati Kamati za
Bunge zilipokaa kujadili taarifa ya Serikali kuhusu Mfumo wa Mapato na
Matumizi, Waziri wa Fedha na Uchumi alitoa Taarifa kuhusu Fedha za Rada
zilizorejeshwa, jumla ya shilingi 72.3 bilioni ambazo zilipokelewa tarehe 26
Machi, 2012. Kwa mshtuko wa Wabunge, Waziri aliiambia Kamati kuwa mchakato wa
manunuzi ya vitabu na madawati kwa kutumia fedha hizi ulikuwa umeanza chini ya Ofisi
ya Waziri Mkuu TAMISEMI. Fedha hizi hazijawahi kupitishwa na Bunge lako tukufu.
Kitendo cha Serikali kuzitumia kabla ya kupitishwa na Bunge ni kuvunja sheria
za Fedha kuhusiana na masuala ya Bajeti. Wakati Waziri akiwasilisha Hotuba yake
hakugusia kabisa suala la fedha zilizorejeshwa kutokana na Ununuzi wa Rada!
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya upinzani
inataka maelezo ya Serikali juu ya Fedha hizi na utaratibu wa kuzitumia. Kambi inataka kufahamu vigezo
vilivyotumika kuteua mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam kutumia fedha
hizi. Kambi pia inapenda kufahamu Deni lililochukuliwa kununua Rada hii
iliyoleta kashfa kubwa sana hapa nchini limefikia kiasi gani kulilipa na
tukililipa tutakuwa tumelipa kiasi gani kwa ujumla.
Mheshimiwa
Spika, Uumbaji wa bajeti ya
Serikali umekuwa ni ule ambao unapendelewa zaidi na wale wavivu wa kufikiri,
yaani mfumo rahisi,
wataalamu wanauita Incremental Budgeting. Mfumo huu hujikita zaidi katika kutizama
ukuaji wa mapato na kugawa mapato hayo kwa mtindo wa nyongeza ya asilimia
Fulani toka katika bajeti iliyotangulia. Mfumo huu huacha kuzingatia mambo
mengi mtambuka. Mfano, tunaweza tizama sekta mojawapo ya umeme ambapo tukifanya
uumbaji wa bajeti kwa mfumo wa kiasi cha nyongeza (incremental budget) kuna
thamani halisi ambazo ukizitizama kwa bei wazi ya soko tayari zimepaa sana
ndani ya miezi kumi na miwili.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
Bungeni, tukiwa ni serikali ambayo tunasubiri kukabidhiwa dola, tunapendekeza
kwamba ni vema tukaanza kutizama uwezekano wa matumizi ya Zero Budgeting ambapo japo ni mfumo ambao unahitaji kazi ya ziada,
lakini una faida sana kwani hutizama mipango ya matumizi kulingana na wakati
uliopo huku ikifanya rejea ya wakati uliopita.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya Upinzani
pia inapendekeza kwamba Bajeti za Mashirika ya Umma ziwe sehemu ya Bajeti Kuu
ya Nchi kwani kuna masuala mengi yanayotekelezwa na Mashirika haya na Wananchi
kupitia Bunge hawayajui. Ni vema katika mfumo mpya wa Bajeti tutakaokuwa nao
kufuatia mapendekezo ya Spika wa Bunge ambapo kutakuwa na Ofisi ya Bajeti ya
Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti, Sheria ya Bajeti (Fiscal Responsibility
Act/Budget Act) izingatie suala la kuziweka kama viambatisho Bajeti za
Mashirika ya Umma katika Bajeti ya Nchi.
Mheshimiwa
Spika, Bajeti ya Serikali ya
mwaka huu kama ilivyowasilishwa na Waziri wa Fedha imewasahau kabisa wananchi
wa vijijini na haina mkakati wowote wa kuwakomboa watanzania walio wengi
wanaoishi huko. Mipango mingi ya kikodi katika sera ya Mapato ya Serikali
itasaidia wakazi wa mijini ambao ni asilimia 25 tu ya Watanzania wote.
Mheshimiwa
Spika, Kambi ya upinzani
inapenda kuweka msisitizo kwamba Tanzania bado ni nchi ya Wakulima maana robo
tatu ya Watanzania wanaishi vijijini ambapo hawajui hizi hadithi za Uchumi
kukua tunazoimba na kupewa sifa kila siku. Hawa ni watu milioni 30 ambao hawana
Maji, hawana Umeme, mazao yao hayafiki sokoni maana hawana barabara nzuri,
shule wanazosoma watoto wao hazina walimu maana wanakimbia mazingira magumu.
Hawa Watanzania wa chini milioni 30 (The Bottom 30M) tunaowawakilisha hawana
bima mazao yakiharibiwa na wala hawana pensheni wanapokuwa wamezeeka na
kupoteza nguvu za kufanya kazi. Hawa ‘The Bottom 30M’ bado wanaishi maisha
walioshi babu zetu. Hawa Watanzania milioni 30 tumewasahau. Tunajenga Mataifa
mawili ndani ya nchi moja, moja la mafukara (wanavijiji) na moja la wanaojiweza
(wamijini).
Mheshimiwa
Spika, Kama tunataka
kujibu kitendawili cha kuwa na Uchumi unaokua kwa kasi lakini haupunguzi
umasikini inabidi kuelekeza nguvu zetu vijijini walipo Watanzania wengi. Kukuza
Uchumi wa Vijijini kwa kuwekeza kwenye misingi ya kujenga uchumi imara ndio
njia pekee ya kutokomeza ufukara wa Watanzania.
Mheshimiwa
Spika, Bajeti Mbadala ya
Kambi ya Upinzani mwaka huu ni Bajeti ya Ukombozi wa mwananchi. Licha ya kwamba tunahitaji ukuaji wa kasi zaidi wa
uchumi. Changamoto sasa ni namna gani ukuaji huu wa uchumi unawafikia wananchi
milioni thelathini wa Vijijini na kuboresha maisha yao.
Mheshimiwa
Spika, KWA KUWA Mpango wa
Maendeleo wa miaka mitano uliwasilishwa Bungeni na Serikali na kupata pongezi nyingi sana kutoka kwa
waheshimiwa wabunge lakini cha kushangaza Serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi imeshindwa
kuutekeleza kwa vitendo mpango huu wa Taifa. Mwaka wa kwanza Mpango haukuwekewa
fedha kwa kuwa ulikuwa wa Mpito. Mpango unahitaji angalau shilingi trillion
Nane kila mwaka ili uweze kutekelezwa.
Mpango ulipata shilingi trillion moja tu mwaka 2011/12.
Mheshimiwa
Spika, KWA KUWA Bunge
liliazimia namna ya kuhakikisha tunapata fedha za kuendeleza nchi yetu sisi
wenyewe, naomba
kunukuu ukurasa wa 92 kifungu cha 4.3.1 katika Mpango wa Maendeleo wa miaka
mitano toleo la kiswahili kama ifuatavyo ‘kwa
kuelewa kuwa wakati wote kutakuwa na miradi ya uwekezaji nje ya mpango,
serikali, kuanzia sasa, itakuwa inatenga asilimia
35 ya makadirio ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kugharamia bajeti ya
maendeleo kila mwaka’ mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa
Spika, KWA KUWA katika
makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/13 Serikali imetenga asilimia sifuri ya Mapato ya ndani kwa ajili ya
kugharamia Bajeti ya Maendeleo. Serikali hii imeshindwa kusimamia ahadi
zake yenyewe kama inavyoonekana katika mpango wa maendeleo ya miaka mitano.
Serikali hii ya CCM imeshindwa kuheshimu Uamuzi uliopitishwa na Bunge kwa
mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Mheshimiwa
Spika, KWA KUWA Kwa mujibu
wa ibara ya 63(3)(c ) madaraka ya Bunge ni pamoja na ‘Kujadili na kuidhinisha
mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika
Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo”.
Bunge liliidhinisha Mpango kwa mujibu wa
ibara tajwa ya Katiba.
Mheshimiwa
Spika, KWA KUWA Bajeti ya
mwaka 2012/13 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi haikukidhi
matakwa ya Mpango wa Maendeleo kama ambavyo ulipitishwa na Bunge, HIVYO BASI,
Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iiondoe
(withdraw) Bungeni Bajeti iliyoileta ili ikatayarishwe upya ili ikidhi matakwa
(compliance) ya Mpango wa Maendeleo kama ulivyoidhinishwa na Bunge na kusainiwa
na Rais wa nchi.
Mheshimiwa
Spika Naomba Kuwasilisha
………………………………………………….
Kabwe
Zuberi Zitto, Mb
Waziri
wa Fedha na Uchumi Kivuli
18.06.2012
SURA
YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA
2012/2013.
|
|
MAPATO
|
%
|
SHILINGI
MILIONI
|
|
|
A
|
Mapato ya ndani
|
57.63
|
|
8,714,671
|
|
|
i)mapato ya kodi (TRA)
|
|
8,070,088
|
|
|
|
ii)Mapato
yasiyo ya kodi
|
|
644,583
|
|
|
B
|
Mapato ya Halmashauri
|
|
362,206
|
|
|
C
|
Mikopo
na Misaada ya kibajeti (GBS)
|
5.57
|
842,487
|
|
|
D
|
Mikopo
na misaada ya miradi ya maendeleo na ya kisekta
|
15.30
|
2,314,231
|
|
|
E
|
Mikopo
ya ndani
|
10.78
|
1,631,231
|
|
|
F
|
Mikopo
yenye masharti ya kibiashara
|
8.25
|
1,254,092
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
JUMLA YA MAPATO YOTE.
|
|
|
15,119,644
|
|
|
MATUMIZI
|
|
|
|
|
E
|
Matumizi ya Kawaida
|
71.06
|
|
10,591,805
|
|
|
(i)
Deni la
taifa
|
|
2,745,056
|
|
|
|
(ii)
Mishahara
|
|
3,781,100
|
|
|
|
(iii)
Matumizi
Mengineyo
|
|
4,065,649
|
|
|
|
Wizara
|
|
3,311,399
|
|
|
|
Mikoa
|
|
49,701
|
|
|
|
Halmashauri
|
|
704,549
|
|
|
H
|
Matumizi ya Maendeleo
|
|
|
|
|
|
(i)Fedha
za ndani
|
|
2,231,608
|
|
|
|
(ii)Fedha
za Nje
|
|
2,34,231
|
|
|
|
Jumla ya matumizi ya maendeleo
|
29.94
|
|
4,527,839
|
|
|
JUMLA YA MATUMIZI YOTE.
|
|
|
|
TOFAUTI
KATI YA BAJETI YA SERIKALI NA BAJETI MBADALA YA KAMBI RASMI YA UPINZANI
|
Bajeti Mbadala ya Kambi ya
Upinzani2012/2013
|
Bajeti ya Serikali kwa
mwaka wa fedha 2012/2013
|
|
Kukuza
uchumi vijijini.
|
Mwelekeo
na malengo ya Serikali hauleweki, hatua zilizochukuliwa ni koboresha uchumi
wa mijini.
|
|
Njia
mbadala zinazotekelezeka za kupunguza mfumuko wa bei.
|
Kuwa
na njia zilezile zilizoshindwa mwaka wa fedha uliopita za kupunguza mfumuko
wa bei.
|
|
Kunufaika
na mapato ya mitaji “Capital gains” kwa kutoza kodi kwa mali za kampuni
zilizopo nchini kwa mauzo yanayofanyika nje ya nchi na hivyo kupanua wigo wa
TRA kutoza kodi
|
Kutoza
hisa kwa mauziano ya hisa pekee kwa mauziano yanayofanyika nje. Hisa
inapunguza wigo wa TRA kutoza kodi.
|
|
Kupanua
wigo wa kodi ya tozo la ujuzi (SDL)kwa kuijumuisha serikali na mashirika ya
umma na kupunguza mzigo kwa sekta binafsi pekee.
|
Kupitia
upya SDL bila kuonyesha namna itakavyofanyika.
|
|
Kupunguza
misamaha ya kodi kutoka 3% ya sasa hadi 1% ya pato la taifa.
|
Kurudia
ahadi zilezile za mwaka jana za kupitia upya misamaha ya kodi bila kuleta
mrejesho wa kile walichokifanya.
|
|
Kuboresha
kodi sekta ya madini ili kupelekea taifa kupata nagalau 25% ya mazuo ya madini nje kama mapato ya
serikali.
|
Kutokuwa
na hatua yoyote ya kuongeza mapato ya Serikali kutoka katika sekta ya madini.
|
|
Kulipa
kima cha chini cha mshahara kuanzia shilingi 315,000.
|
Kulipa
shilingi 170,000 kama kima cha chini.
|
|
Kulipa
pensheni kwa wazee wote kuanzia miaka 60 na kuendelea
|
Kutokuwa
na mfumo wa pensheni kwa wote.
|
|
Kushusha
kiwango cha chini kodi ya mapato kwa wafanyakazi (PAYE) kutoka 14% hadi 9% ili kumpunguzia mfanyakazi makali ya maisha
na kutoza kodi zaidi kwa watu wenye kipato kikubwa
|
Kubaki
na kiwango kilekile cha chini cha kodi ya 14% na kubakiza mfumo ule ule wa
kodi ya Mapato unaomfanya Masikini alipe zaidi ya Tajiri.
|
|
|
|
|
Kuziba
mianya kwa makampuni ya simu kukwepa kutokulipa kodi ya mapato.
|
Kuongeza
ushuru wa bidhaa kwenye muda wa maongezi na hivyo kumwongezea gharama
mwananchi.
|
|
Kuondoa
mikopo ya kibiashara ili kulipunguzia taifa mzigo wa madeni
|
Kuendelea
mikopo na hivyo kuongeza deni la taifa. mingi ya kibiashara.
|
|
|
|
|
Kutenga
asilimia 35 ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo kama ilivyoelekezwa kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
|
Kutenga
asilimia sifuri ya fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo
na hvyo kutokutekeleza mpango wa taifa .
|
|
Utegemezi
wa Bajeti 21.3%
|
Utegemezi
wa Bajeti 42.37%
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
JEDWALI
LA ULINGANISHO WA ASILIMIA KWA BAJTEI MBILI
|
|
UPINZANI
|
ASILIMIA
|
SERIKALI
|
ASILIMIA
|
|
|
Mapato
ya ndani
|
78.70
|
Mapato
ya ndani
|
57.63
|
|
|
Mikopo
na Misaada ya kibajeti (GBS)
|
5.57
|
Mikopo na Misaada
ya kibajeti (GBS)
|
5.57
|
|
|
Misaada
na mikopo ya miradi ya maendeleo na y a
kisekta
|
15.30
|
Misaada
na mikopo ya miradi ya maendeleo na y a
Kisekta
|
15.30
|
|
|
Mikopo ya
masharti ya kibiashara ya ndani
|
0
|
Mikopo ya
masharti ya kibiashara ya ndani
|
10.78
|
|
|
Mikopo ya
masharti ya kibiashara ya nje.
|
0
|
Mikopo ya
masharti ya kibiashara ya nje.
|
8.25
|
|
|
Matumizi ya Kawaida
|
59.22
|
Matumizi ya Kawaida
|
71.06
|
|
|
Matumizi ya Maendeleo
|
40.78
|
Matumizi ya Maendeleo
|
29.94
|
|
|
Matumizi ya
maendeleo fedha za mapato ya ndani
|
36.06
|
Matumizi ya
maendeleo fedha za ndani
|
0
|
|
|
Matumizi ya
maendeleo fedha za nje
|
12.39
|
Matumizi ya
maendeleo fedha za nje
|
29.94
|
No comments:
Post a Comment