Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika
mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio
zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo
mbalimbali za kimataifa.
Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama
vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight, na nyingine
nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii
wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika
jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York
City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na
kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.
eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara
tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama
Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani wengine
kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea
kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana
katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon
mwaka jana.
Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances
ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa
pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss
Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja
kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa
wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati
ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.
Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club
mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42.
Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa
watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote
wanaweza kukimbia.
No comments:
Post a Comment