MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Monday, July 9, 2012

Rais Kikwete amkabidhi mama Maria Nyerere Tuzo ya Heshima ya Taifa la Burundi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mama Maria Nyerere Tuzo ya Juu ya Heshima ya Taifa la Burundi aliyotunukiwa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Burundi yaliyofanyika mjini Bujumbura wiki iliyopita.Mwalimu Nyerere alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Burundi ambapo alikuwa mshauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Kwanza wa nchi hiyo Prince Louis Rwagasore. Rais Kikwete alimkabidhi Mama Maria tuzo hiyo leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.   

No comments:

Post a Comment