HATIMAYE vivutio vitatu vya kitalii vya nchini Tanzania vimefanikiwa
kuingiza katika maajabu Saba ya Bara la Afrika.
Vivutio vya kitalii vilivyoshinda na kuingia maajabu Saba
ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Creater na mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Sherehe za kutangaza vivutio vilivyoshinda ilifanyika jana
jijini Arusha na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye aliyekuwa mgeni rasmi ambapo
wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi walihudhuria.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa maajabu hayo Pinda
aliwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kuvitangaza na kuvienzi vivutio hivyo ili
vizipoteze sifa yake.
“ Changamoto iliyopo mbele yetu ni kuhakikisha vivutio hivi
vilivyoshinda na vingine tuna vilinda na kuvitunza ili visiendelee kupoteza
sifa,” alisema Pinda.
Akizungumzia maajabu ya Hifadhi ya Serengeti Pinda alisema,
hifadhi imefanikiwa kuingia na kushinda katika maajabu Saba ya Afrika kutokana
na upekee wake wa kuwa na histori ya aina yake.
Aliitaja historia hiyo kuwa ni pamoja na kuwa na sifa ya
kipekee inayotambulika kama sehemu ya urithi wa dunia iliyopo chini ya UNESCO,
ikiwa pia na wanyama aina ya Pundamilia takribabni 200,000 na Swala takriban 300,000.
Kwa upande wa Mlima Kilimanjaro Pinda alisema kivutio hicho
kimefanikiwa kushinda kutokana na kuwa ndio Mlima mrefu pekee barani Afrika
ukiwa pia ni sehemu ya urithi wa dunia inayotambuliwa na UNESCO.
Pinda aliendelea kubainisha kwamba kwa upande wa Ngorongoro
pamoja na kuwa ipo ndani ya sehemu ya urithi wa dunia inayotambuliwa na UNESCO
pia ndio sehemu pekee duniani ambayo wanyama wa porini wanaishi kwa
kuchanganyika na binadamu na wanyama wa kufungwa.
Katika hatua hiyo Pinda aliwashukuru Watanzania na Shirika
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kuvipigia kura vivutio hivyo na hatimaye
kuweza kufanikiwa kuingia katika maajabu Saba ya dunia.
Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Maajabu Saba ya Dunia
Dk. Phillip Imler akitangaza vivutio vingine vilivyoshinda baada ya kupigiwa
kura ambapo alivitaja kuwa ni pamoja na Mto Nile, Red See Reefs, Sahara Desert
na Olevango Delter iliyopo nchini Botswana.
Pamoja na wageni kutoka nje ya nchi baadhi ya wageni
wengine waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na wabunge, wakuu wa wilaya na
watendaji na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini.
No comments:
Post a Comment