Washiri wa shindano la Miss Utalii Taifa wakiwa katika picha ya pamoja
Bendi ya Akudo Impact wazee wa
masauti ,siku ya Jumapili tarehe 17, Februari 2013, itatoa burudani katika shindano
la Taifa la kumsaka Mrembo wa Utalii mwenye kipaji kati ya warembo 40 waliopo
kambini Ikondelelo Lodge wakijiandaa kushiriki Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania 2012/13 zitakazo fanyika mwisho wa mwezi huu katika Ukumbi wa Dar Live
jijini Dar es Salaam.
Katika shindano hilo la Vipaji ,
ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Jeshi wa Msasani Beach Club Jumapili
kuanzia saa nane mchana ,pamoja na Bendi hiyo ya Akudo Impact , wasanii wengine
watakao tumbuiza ni pamoja na mwanamuziki wa kimataifa Che Mundugwao, Msanii
mdogo chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Geneous na burudani za ngoma za asili
kutoka katika kundi kongwe la Kaole
Sanaa Group wakiomgozwa na mwana dada mahili katika uchezaji wa ngoma za
asili Mariam Kweji aka kalunde wa Bongo Movie.
Shindano hilo la Vipaji ni moja ya
mashindano ya awali ya kuwania tuzo mbalimbali kabla ya Fainali kuu,ambapo
washiriki wote watashindana kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila
mbalimbali ya mikoa wanayo iwakilisha. Mikoa hiyo na majina ya washiriki katika
mabano ni Arusha (Rose Godwin), Dar es
Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine
Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob),
Kagera 1(Elline Bwire), Kagera2 (Jania
Abdul), Kagera 3(Mulky Uda), Kilimanjaro
(Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis),Mara (Dorine Bukoni),
Manyara (Mary C. Lita), Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro
(Hadija Said),Tanga (Sarafina Jackson), Ruvuma 2 (Leah Makange), Tabora
(Magreth Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi
(Asha Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma
(Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani
(Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu
(Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange)
Wakizungumzia kwa nyakati tofauti
shindano hilo la Vipaji,Rais wa Miss Tourism Tanzania International
Organisation ,wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo ,
alisema kuwa mandalizi karibu yote yamekamilika kuanzia ngazi za warembo hadi
burudani za bendi, ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya. Hili litakuwa ni
tukio kubwa na la kihistoria kuwahi kufanyika Tanzania ambapo Utalii, Urembo na
Utamaduni wa ngoma za asili vitaonyeshwa kwa pamoja jukwaani, lakini kivutio
cha pekee ni jinsi mabinti wa kizazi kipya tena warembo kutoka mikoa yote ya
Tanzania na vyuo Vikuu watakavyo onyesha maajabu ya kusakata ngoma za asili kwa
umahili mkubwa na wa pekee.
Shindano la Miss Utalii Tanzania
mwaka huu limedhaminiwa na wadhamini mbalimbali wakiwemo Coca Cola Kwanza
Limited, Daja Salon, Mtwana Catering Services Enterprises, Zizzu Fashion,
Global Publishers, Ikondelelo Lodge, Clouds Media Group, Tone Multimedia Group,Valley
Spring na www.misstourismorganisation.blogspot.com
Katika Shindano hili viingilio
vitakuwa ni kama ifuatavyo 5,000 kwa viti vya kawaida, 10,000 kwa V.I.P 2, na
30,000 kwa V.I.P 1 pamoja na Chakula.
No comments:
Post a Comment