NA. BENEDICT LIWENGA-MAELEZO-Dar.
Serikali ya Japan kupitia Shirika
la JICA imesaini mkataba wa kuisaidia
Tanzania shilingi Bilioni 1.28 za kusaidia
usambazaji maji katika mkoa wa Tabora .
Fedha hizo zimetolewa leo(jana)
na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mh. MASAKI OKADA katika sherehe iliyofanyika
jijini Dar es salaam.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya
Tanzania Waziri wa Fedha Mh. Dkt. William Mgimwa alisema msaada huo utasaidia
kupunguza kero ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya vijiji mkoani Tabora na
pia kukabiliana na vita dhidi ya umaskini.
‘’Ninafurahi ya kuona kwamba
makubaliano ya msaada huu tulio saini hivi punde utaiwezesha serikali yako ya
Japan kupitia kampuni ya JICA kutupatia fedha za Kijapan Yeni 76 milioni sawa
na shilingi bilioni 1.28 za kitanzania, kwaajili ya kusaidia utekelezaji wa
usamabazaji maji vijijini katika mkoa wa Tabora”. Mh. Dkt, Mgimwa alisema.
Aidha Dkt Mgimwa kwa niaba ya Serikali
ya Jamuhuri ya Tanzania aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaada wake huo muhimu ambao umekuja muda muafaka wakati Tanzania iko katika
mapambano dhidi ya umaskini ikiwemo kuhakikisha wanapata maji safi na salama.
Kwa upande wake Balozi wa Japan
nchini Tanzania Mh, MASAKI OKADA alisema kuwa Japan tangu mwaka 1996,inatekeleza miradi sita ya maji katika
mikoa ya Kagera ,Singida, Manyara , Shinyanga ,Mwanza , Mara, Mtwara , Lindi,
Pwani , Dar es Salaam pamoja na Zanzibar.
Alisema kuwa hadi hivi sasa jumla
ya watu laki nane na sitini elfu wamenufaika na miradi hiyo hapa nchini Tanzania.
Japan na Tanzania zimekuwa na
uhusiano wa muda mrefu ambapo hadi hivi sasa uhusiano wa Nchi hizo umedumu kwa
muda wa miaka 50
No comments:
Post a Comment