MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Sunday, March 31, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MKEWE WAWAJULIA HALI WALIONUSURIKA KUANGUKIWA NA JENGO LAGHOROFA 16 DAR ES SALAAM

Rais Jakaya  Kikwete ametembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili  kuwapa pole majeruhi walioumia katika ghorofa lililoporomoka juzi Ijumaa Machi 26, 2013 katika Mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 20.
Rais Kikwete, akiwa ameongozana na mke wake, Mama Salma Kikwete, pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),  Hawa Ghasia, aliwatembelea na kuwapa pole majeruhi Mohamed Ally Dhamji, Baqir Virani, Selemani Saidi na Yusuf Abdallah  waliolazwa Taasisi ya Mifupa (MOI).
Majeruhi hao, ambao kwa mujibu wa Daktari C.N. Mcharo wanaendelea vyema na matibabu na hali zao ni za kuridhisha, ni wanne na kati ya sita waliolazwa katika taasisi hiyo, ambapo wawili wamekwisharuhusiwa.
 









No comments:

Post a Comment