Wabunge wa Chama cha CUF wameleta tafrani Bungeni mjini Dodoma leo wakati Mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje, akisoma hotuba ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wenje akiendelea kusoma hotuba hiyo ndipo Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdalla Salim, aliomba muongozao kwa Naibu Spika, Job Ndugai akipinga maneno yaliyokuwa yameandikwa ukrasa wa nane wa hotuba hiyo yaliyosome kama ifuatavyo, Mheshimiwa Spika wa Upande wa CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na kupigania haki za ndoa ya Jinsia moja, usagaji na ushoga hii ni kwa mujibu wa tangazo lao la kwenye mtandao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, ikiungwa mkono na Waziri wa Haki na usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka Chama cha LiberaDemocratis wakati Chama hicho (www.libera-international.org)
Baada ya hapo wabunge wa Cuf walitaka maneno hayo yafutwe ingawa msomaji wa hotuba hiyo alikuwa hajafika katika ukrasa huo wa hotuba wakati akisoma, yeye alikuwa ukrasa wa nne
Baada ya kuhisiwa vurugu ingekuwa kubwa naibu Spika , Job Ndugai alitumia busara zake za kusitisha shughuri za Bunge kabla mambo hayajawa mabaya maana kulikuwa na dalili za kuanza kushikana mashati baada ya baadhi ya wabunge wa Chama hicho kuanza kufoka kwa sauti kubwa ndani ya Bunge
No comments:
Post a Comment