Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga.
Ndugu
wananchi,
Jumatano tarehe 5 Juni, 2013 Watanzania tutaungana
tena na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Mazingia Duniani. Siku ya tarehe 5 Juni iliamuliwa kuwa Siku ya
Mazingira Duniani kwa Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972 ikiwa ni
kielelezo cha ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu
Mazingira uliofanyika huko Stockholm, Uswidi.
Aidha, Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa
Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, yaani UNEP, pia lilipitishwa siku
hiyo. Kama mnavyojua, UNEP ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa chenye makao
makuu yake katika bara la Afrika, huko Nairobi Kenya. Tangu tarehe 5 Juni, 1973,
nchi mbalimbali zaidi ya 140 huadhimisha siku hii kila mwaka.
Lengo letu kubwa katika kuadhimisha siku hii kama Taifa
ni kuweka msisitizo katika masuala ya mazingira na kuwapa uwezo wananchi ili
wawe mawakala wazuri wa maendeleo endelevu.
Vile vile maadhimisho haya hutoa nafasi muhimu ya kutafakarikuhusu hali
na umuhimu wa mazingira kwa nchi yetu, kuelimishana na kukuza ari ya wananchi
kushiriki katika shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira yao.
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kitaifa
kwa mwaka huu yatafanyikia Mkoani Rukwa, na kimataifa yatafanyikia nchini Mongolia.
Ujumbe wa mwaka huu wa Siku ya Mazingira Duniani ni:
“Fikiri, Kula: Hifadhi Mazingira” au kwa lugha ya
Kiingereza ”Think – Eat – Save”. Ujumbe huu unatukumbusha na kutuhimiza
tutimize wajibu wetu ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa shughuli tunazofanya za
uzalishaji mali na utoaji wa huduma zinakuwa rafiki wa mazingira na zisiwe chanzo cha uharibifu wake. Hapa nchini ujumbe unaoongoza maadhimisho ya
mwaka huu ni “Fikiri, Kabla ya Kula: Hifadhi Mazingira”
Ndugu
wananchi,
Madhumuni yangu leo ni kuwaombeni wananchi wote
kuienzi Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya yafuatayo:-
Þ
Kufanya usafi
kwenye maeneo ikiwa ni pamoja na kufagia na kuzoa taka na kuzitupa kwenye
maeneo yaliyotengwa,
Þ
Kufyeka
vichaka vinavyozunguka makazi yetu,
Þ
Kuchimba vyoo
vya kudumu na kuvitumia,
Þ
Kuzibua
mifereji na mitaro ya maji taka,
Þ
Kufukia madimbwi
ya maji,
Þ
Palipo na mvua
na maji ya kutosha, kupanda nyasi na miti inayofaa kwenye maeneo
yanayotuzunguka hasa yale maeneo kame,
Þ
Kusafisha
visima na vyanzo vya maji,
Þ
Kusafisha
maeneo ya maji kwa ajili ya mifugo, na
Þ
Kutoa zawadi
kwa washindi wa mashindano ya usafi wa miji na majiji chini ya utaratibu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Ndugu
wananchi,
Katika kutekeleza hayo niliyoyataja, wananchi
mnayo nafasi ya kuchagua aina ya mchango wa ushiriki wenu katika sherehe hizi,
na namna mtakavyoona inafaa kuutoa. Vile
vile napenda kutoa wito kwenu wananchi
wote mnaoishi mjini na vijijini, mashirika ya umma, mashirika ya kiserikali na
yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi, viwanda na taasisi za elimu na utafiti
kushiriki katika maadhimisho haya katika maeneo yenu. Jukumu la hifadhi na usalama wa mazingira ni
letu sote, wazee kwa vijana, wake kwa waume.
Mafanikio yatatagemea juhudi za kila mmoja wetu anavyoshiriki katika
shughuli za kuhifadhi mazingira. Natoa
wito kwamba, kuanzia tarehe 1 hadi 4 Juni, ziwe ni siku mahsusi kwa ajili ya
kufanya shughuli za usafi na shughuli
nyinginezo zinazolenga kulinda na kuhifadhi ya mazingira ya makazi yetu, mitaa
inayotuhusu, vijiji vyetu, miji na majiji yetu.
Baada ya kusema haya, napenda kutumia nafasi hii
kuwashukuru sana wale wote ambao wamejipanga kutekeleza shughuli mbalimbali za
kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Naushukuru uongozi wa mkoa wa Rukwa, kwa kukubali kuwa mwenyeji wa maadhimisho
haya kitaifa. Pia nazipongeza Halmashauri
za wilaya na Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Taasisi na wananchi wote kwa
ujumla kwa ushirikiano wanaouonesha katika maandalizi ya maadhimisho haya.
No comments:
Post a Comment