Biashara Na Maonesho ya Harusi
Watu wengi zaidi wahamasishwa kushiriki na kutembelea
Maandalizi ya Harusi Fashion Show 2013 yapamba moto, Maonesho
hayo ya mavazi na wafanyabiashara wa bidhaa na huduma za harusi yanatarajiwa
kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Dar es
salaam. Muanzilishi na muandaaji wa Harusi Fashion Show Mustafa Hassanali
amesema ikiwa ni mwaka wake wanne maonesho haya yamekuwa na kuongezeka ubora
ukilinganisha na miaka iliyopita halikadhalika tunatarajia kuona mabadiliko
kwenye tasnia ya Harusi na washikadau wake.
Mwaka huu Harusi Fashion Show tayari
imeshawavuta washiriki wengi, wengi wao
ni washiriki ambao wapo toka kuanzishwa kwa maonesho haya mwaka 2010.
Maonesho haya yanatarajiwa kufanyika
kuanzia saa moja kamili joini na kuendelea.
“Harusi ni muunganiko wa familia na
jamii na nikumbukumbu muhimu ya itakayodumu maisha yote, hivyo basi tumeamua
kuwapa bibi na bwana harusi watarajiwa mahitaji yao
yote ya siku hiyo muhimu kwenye hitoria ya maisha yao.” Amesema ndugu Esi Mgimba Afisa Habari
na Mahusiano wa 361 degrees ambao ndio waandaaji wa onesho hilo.
Harusi Fashion Show inawaleta pamoja
wadau wa biashara za harusi ili waweze kukutana kufahamiana na kuangalia fursa
za kibiashara baina yao ili waweze kuzitumia kuboresha biashara zao na uhusiano
wa kibiashara ambao utachangia kukuwa
kwa tasnia hii.
Miongoni mwa washiriki amabao
watakuwepo mwaka huu ni pamoja na keki, maua
na wapambaji, wapiga picha, wabunifu wa mavazi ya harusi na wengineo wengi.
Na wafuatao ni washiriki wa Maonesho ya
Harusi Mwaka huu,
The Wedding Kingdom, Sintah Bridal
Lounge, E-cakes, Twaiba Classic, Manjou, An Nisaa Abayas, Mustafa Hassanali
Bridals, Queen Jeweler, Mbezi Beach Hotel, Malaika Media, Harusi Nzuri, Julius
Importers and Exporters Ltd, Rupam Stores, AVP, Shyland Photogenic, Gogo Shop,
Liquid Lab, Brand House, The Cake Shop, Van Roy Production, Eve Collection na
East West Photography.
“Kwakuwa idadi kubwa ya washiriki
imethibitisha ushiriki wao, viingilio kwenye maonesho ya harusi ni 50,000 kwa
viti maalumu na 20,000 kwa viti vya kawaida, na kutazama vipambio vya harusi ni
bure, tunawaomba na kuwashauri watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kuona na
kuthamini ubunifu wa bidhaa za Kitanzania “ alimalizia ndugu Mgimba.
Maonyesho hayo ya biashara za Harusi
yameletwa kwenu kwa hisani ya 361 degrees, Clouds Fm and Clouds Tv, Eventlites,
Prime advitising, Century Cinemax na
Baileys Cream with Spirit.
No comments:
Post a Comment