BBC
Kunako siku ya mwisho kwa vilabu vya mpira wa miguu
kukamilisha usajili wa wachezaji klabu ya Arsenal imeafikiana na
mchezaji Mesut Ozil wa Ujerumani anayechezea klabu ya Real Madrid kwa
kitita cha pauni za Uingereza milioni £42.4.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, klabu ya
Arsenal imekubaliana na Real Madrid kuilipa pauni za Uingereza milioni
£42.4m sawa na Euro milioni 50 kumsajili Mjerumani Mesut Ozil.
Kijana
huyo menye umri wa miaka 24 amefikia makubaliano na Arsenal kuhusu
maslahi yake binafsi ingawa sharti apitie mchakato wa vipimo vya afya
yake kabla ya Arsenal kukamilisha usajili ambao katika historia ya klabu
hio haujawahi kufanyika kumsajili mchezaji kwa zaidi ya pauni milioni
22.
Kwa wakati huu Ozil yuko pamoja na kikosi cha Timu ya Taifa ya Ujerumani na itabidi afanyiwe vipimo huko huko Ujerumani.
Kwa kipindi cha msimu wa likizo na usajili wa
wachezaji Arsenal imeshindwa kuwasajili wachezaji wa kiwango
anachokitaka Arsene Wenger kama mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na
Gonzalo Higuain, mchezaji mwingine aliyekua huko Real Madrid.
Lakini kwa sasa yumkini Ozil anaelekea uwanja wa
Emirates kufuatia usajili wa Gareth Bale kwa kitita kikubwa cha pauni
milioni 85.3.
Kabla ya kujiunga na Real Ozil alikua akichezea
klabu ya Werder Bremen alikosajiliwa na Real kwa takriban pauni milioni
12.4 na kuichezea Real mara 155.
Wakati Arsenal ikijitahidi kusajili kabla ya
dakika ya mwisho ya shughuli ya usajili Liverpool pia imetiliana saini
na Mamadou Sakho na Tiago Ilori kwa jumla ya pauni milioni 25.
Sakho mwenye umri wa miaka 23 ameichezea Timu ya
Taifa ya Ufaransa mara 14 France na amegharimu pauni milioni £18m
kutoka klabu ya Paris St-Germain.
Ilori alizaliwa mjini London na ameiwakilisha Timu ya Ureno ya vijana ingawa bado anaweza kuiwakilisha England.
Liverpool haikuishia hapo ila imemzoa Mnaijeria Victor Moses kutoka Chelsea.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao 10 akishiriki
mechi 42 za Cheslea lakini amekabiliwa na ushindani mkali wa kuweza
kuingia uwanjani kufuatia usajili wa mcheza kiungo kutoka Brazil
Willian, Mjerumani Schurrle pamoja na mkongwe wa Cameroon Samuel Eto'o.
No comments:
Post a Comment