Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na
Yanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 18 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000.
Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa
upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi
ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B
itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja
itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo
hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa
Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza
Madukani.
Mechi
hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam,
ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na Ferdinand
Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati mtathmini wa
waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
No comments:
Post a Comment