Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili
mjini Njombe jana, Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja
kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni
mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo
ya kwanza tokea Njombe kutangaza kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika
siku yake ya kwanza leo Oktoba 18, mbali na kuzindua Mkoa wa
Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na
wananchi.
Katika
ziara hiyo ambako pia Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni
Njombe, Wanging’ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha,
Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa
Liganga.
No comments:
Post a Comment