Kufuatia gumzo iliyokuwa imetanda ya mchezo kati ya Mbeya City na Azam FC jana mashabiki wengi walikacha kwenda kushuhudia mpambano wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania kati ya Yanga ya Dar es Salaam inayoongaza ligi na timu ya Jeshi ya JKT Orjolo ya jijini Arusha na kukumbilia Uwanja wa Azam Complex kwenda shuhudia mchezo huo wa Mbeya City na Azam FC, Si Kawaida Uwanja wa Taifa kuoneka ukiwa mweupe namna hii wakati Yanga ikicheza lakini jana mashabiki wengi walikacha na kwenda Chamaz
Wakati huohuo Yanga sasa imemaliza Mzunguko wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kukali kiti cha usukani baada ya kuibanjua timu ya Jkt Orjolo bao 3-0 kwa bila wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam
Simon Msuva ndiye alikuwa wa kwanza kuandika baom, akifuatiwa na Mrisho Ngassa aliyachia shuti kali la umbali wa mita zaidi ya 18 baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa timu yaJkt Orjolo na baadaye kipindi cha pili Jerson Tegete aliyeingia kipindi cha pili aliweza kuhitimisha kwa kufunga bao la tatu.
Simon Msuva (kulia) na Khamis Kiiza wakishangilia bao la kwanza.
Simon Msuva (kulia) na Khamis Kiiza wakishangilia bao la kwanzaMrisho Ngassa mbele, Simon Msuva na Frank Domayo akishangilia bao la pili
No comments:
Post a Comment