MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Saturday, March 8, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE

Hakuna asiyefahamu kwamba mwanamke ni nguzo kuu katika familia, ndiye mlezi na mwangalizi mkuu wa watoto na mfanyaji kwa ujumla.
 
ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani jamii lazima ibadilike na kumsaidia sana mwanamke kutokana na kuwa na kazi nyingi anazopaswa kuzifanya kwa siku
 
mwanamke wa kijijini ndiye nguzo kuu ya familia, ukimwesabia kazi azifanyazo kwa siku unaweza ukafikiri kwama kesho yake hatafanya kazi tena lakini kwa sababu mwanamke mwenyewe anatambua wajibu wake ni inamlazimu afanye hizo kazi kwa kujituma
 
mwanamke sasa wakati umefiki wa kukombolewa na kusaidiwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na wanaume
 
Mama wa kijijini sijui kama anafahamu hata hii siku ya sherehe za wanawake duniani maana anavyokuwa ni mtu wa kazi kila kukicha ni mara chache sana kumkuta mwanamke wa kijijini naye anapata muda angalau wa kujipumzisha
 
maana yeye kila kukicha na kazi na yeye, asubuhi atawandaa watoto kwenda shule, hapo bado hajafwata maji umbali wa kilomita zisizopungu mbili, baada ya hapo aende shamba na umbali wa Shambani mfupi ni kilomita tano, baada ya kazi ya shamba, atafute kuni hapo bado ya kazi ya kuanndaa chakula inamsubiri yeye mwamamke
 
Hapa lazima elimu inahitaji kutoa elimu ili jamii iweze kubadilika na kuweza kusaidiana ili ujenzi na utengeneza na ulinzi wa watoto uende pamoja

No comments:

Post a Comment