Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, Profesa John Nkoma leo katika Mkutano na waandishi wa habari pamoja na wamiliki wa Makampuni ya Simu za mikononi ametangaza kuongezwa muda wa usajili wa simu.
Akizungumza katika Mkutano huo Prosea alisema wamezingatia mambo mengi mpaka kufikia uamuzu huo ikiwa ni pamoja na watu wanaoishi vijijini au sehemu zisizofikika kiurahisi ikiwa ni pamoja na sehemu zisizo patikana umeme ,kwamba wamegundua hata kutoa kopi ya kitambulisho ni tatizo kwa hiyo wamefia uamuzi huo ili watu wa makampuni ya simu wajipange tena katika swala hilo
kwa hiyo zoezi la kusajili simu litakwenda mpaka mwezi wa sita mwakani. Hata hivyo watanazania wanaendelea kuhimizwa katika zoezi hilo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
No comments:
Post a Comment