MDAU POPOTE ULIPO TUMA PICHA NA HABARI KWA E-mail:  antonysiame74@yahoo.com

Thursday, May 19, 2011

TBL YAPATA TUZO

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imeibuka mshindi wa jumla wa tuzo ya masoko, mauzo na usambazaji ya makampuni ya SABMiller katika hafla fupi iliyofanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurungezi wa Masoko wa TBL, David Minja, alisema kampuni yake ilishinda tuzo hizo zilizoshirikisha nchi tisa.
Nchi nyingine zilizoshiriki tuzo hiyo mbali ya Tanzania ni; Uganda, Msumbiji, Ghana, Nigeria, Zambia, Lesotho, Swaziland na Botswana.

Mbali ya kushinda tuzo katika maeneo hayo matatu, Minja alisema kwamba upande wa masoko walitwaa tuzo tatu pekee.

“Tumeshinda tuzo tatu za masoko kwa kutambua juhudi mbalimbali zinazosaidia kukuza soko,” alisema.

Alizitaja juhudi hizo kuwa ni; kujenga soko tofauti kwa bidhaa za TBL, kujenga soko tofauti kwa bidhaa za TBL kitaifa na kimataifa kwa kupitia bia ya Ndovu Special Malt na Tuzo ya Masoko bora kiutendaji.
Kwa upande wa tuzo ya mauzo na usambazaji, TBL ilijinyakulia tuzo ya dhahabau ya mkurugenzi Mtendaji wa SABMiller Afrika kama timu bora ya mauzo na usambazaji kwa mwaka 2011, alisema.
Tuzo hizo, Minja alikabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SABMiller Afrika, Mark Bowman.

SABMiller ni moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano.

No comments:

Post a Comment