Baada ya mashabi wa Simba kulalamikia kitendo cha mwandishi mpiga picha kukaa upande wao huku akiwa amevalia T-Shirt yenye rangi ya jano walianza kupiga kelele ili aondolewe eneo hilo, Hapa kamanda wa polisi akizungumza na Joseph Senga kwamba mashabiki wa Simba hawataki ukae huku ndugu
Huku inabidi uondoke kwa usalama wako
Nenda upande wa kule walikokaa wenzako wa Yanga kaka
Mbona mi ni mwandishi na kitambulisho hiki kamanda
wapiga Picha baada ya kuona hivyo wakaona ni tukio wakachangamkia kupiga picha
kabla ya kuondolewa na Askari alifuatwa na mmoja wa maofisa wa maswala ya usimamiaji wa michuano hiyo
Ndugu yangu nyanyuka watakupiga na chupa za maji
Niache nitarudi kule nilikokuwa kwa wenzangu
Ngoja nitoe kitambulisho basi maana tunakoelekea siko Kamanda
we twende tu
Mmmmm lakini hamjanitendea haki mimi ni mwandishi wa siku nyingi hawa mashabiki wananielewa wengine ni watoto wangu jamani
No comments:
Post a Comment